Mgombea ubunge wa Jimbo la Sikonge, George Kakunda akiwahutubia
wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Kata ya Mabama,
Mkoa wa Tabora leo.[/caption]
MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Mama Samia Suluhu Hassan amesema endapo chama chake kitafanikiwa
kushinda na kuunda Serikali kitahakikisha vyama vyote vya ushirika vya
wakulima vinaangaliwa upya ili kuhakikisha vinawasaidia wakulima.
Alisema wapo baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika ambao wanavitumia
vibaya vyama vya ushirika na kuwanufaisha zaidi wao zaidi ya wakulima
jambo ambalo limekuwa halina manufaa kwao. "...Tutaviangalia upya vyama
vyote vya ushirika ili kuhakikisha tunaweka viongozi wenye utashi
wanaoweza kuwanufaisha wakulima, maana wapo baadhi ya watu ambao
wanajifanya mungu watu...wanataka wao waabudiwe hili halikubaliki hata
kidogo," alisema mgombea mwenza.
Mama Samia Suluhu alisema wamepanga kuiongezea uwezo taasisi
iliyoanzishwa kwa ajili ya kushughulikia kero anuai za walimu ili iweze
kuangalia masuala kama viwango vya mishahara ya walimu, upandishaji
madaraja na vyeo vya walimu pamoja na maslahi mengine ya wafanyakazi.
Alisema Serikali ya CCM itahakikisha maslahi ya wakulima na wafanyakazi
yanaangaliwa kwa karibu kupitia taasisi maalumu ili kuchochea ufanisi na
uwajibikaji kazini. Alisema ni jambo la kushangaza kuona wakulima
wanalima mazao yao na baadaye kulipwa kwa taabu huku wakiwa wametumia
gharama zao.
Kwa upande wake aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini
kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Daudi
Nteminyanda aliwaomba wananchi kukinyima kura chama hicho kwani hakina
viongozi waadilifu zaidi ya viongozi maslahi. Alisema viongozi wa
CHADEMA ni vigeugeu ambao hawapaswi kupewa uongozi wa nchi kwa kile
kuwakumbatia watu kiliokuwa kikuwaita mafisadi hapo awali lakini leo
kimewapa nyazifa za juu.
Kiongozi huyo wa Chadema ambaye alishinda kura za maoini katika nafasi
yake na baadaye kukatwa nafasi yake kisha kupewa aliyekuwa kada wa CCM,
Josef Kidaha aliyehamia Chadema kwa sasa amekikimbia chama cha Chadema
na kujiunga na CCM, huku akikinadi ndiyo chama pekee shupavu
kitakachoreta maendeleo.
Mama Samia Suluhu leo amemaliza ziara ya kampeni Mkoani Tabora baada ya
kufanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Urambo Magharibi, Urambo
Mashariki, Tabora Kaskazini-Uyui, na Jimbo la Sikonge. Kesho anaelekea
Mkoa wa Kigoma kuendelea na ziara yake ya kampeni kunadi ilani ya CCM.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Kata ya Mabama, Jimbo la Sikonge Tabora. |
Wagombea nafasi ya udiwani kupitia CCM Sikonge wakiwa katika mkutano wa hadhara jimboni humo. |
Mgombea ubunge wa Jimbo la Urambo Magharibi, Magreth Sitta akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Jimboni humo Mkoa wa Tabora leo. |
Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi wenye vizibau wakiwa katika moja ya mikutano ya kampeni za CCM leo. |
Kundi la wasanii wa Bongo Movie makada wa CCM wakiwaburudisha wananchi katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM Jimbo la Urambo Mashariki Wilaya ya Kaliua leo. |
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Sikonge, Said Nkumba akiwa meza kuu katika mkutano wa kampeni wa CCM leo katika Kata ya Maboma. |
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269