NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
………………………………………………..
MGOMBEA Urais kupitia tiketi
ya Chama cha mapinduzi (CCM) Dr. John Magufuli amewahakikishia
wananchi wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani endapo akipewa lidhaa ya
kuongoza nchi ni lazima atimize azma yake ya kuimarisha miundombinu ya
barabara kwa kujenga njia sita za lami kuanzia Jijini Dar es Slaam
kupitia maeneo ya , mlandizi, chalinze mpaka mkoani morogoro ili
kuondokana na changamoto ya msongamano wa magari.
Magufuli aliyasema hayo wakati
wa alipofanya mikutano yake miwili ya hadhara katika jimbo la kibaha
vijijini pamoja na jimbo la kibhaa mjini ambapo alidai kuwa ana imani
miundombinu ya baarabara ikitengenezwa katika kiwango kinachotakiwa
kinatweza kuleta fursa ya wafanyabishara kusafirisha mizigo yao na
biashara kwa urahisi na kuweza kukuza uchumi.
Aidha Magufuli alisema kwamba
lengo lake kubwa ni kuhakikisha anapamabana kufa na kupona ili kuweza
kuondoka na msongamano wa foleni ya magari ambao umekuwa ni kero ya
siku nyingi katika barabara ya morogoro hivyo kukamilika kwa ujenzi huo
wa njia nsita kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa waananchi wa kibaha
pamoja na Taifa zima kwa ujumla.
“Mimia hapa napenda
kuwahakikishia wananchi wa kibaha kwa kushirikiana na Silvestry koka
kuwa hii kero ya msongamano ya magari katika barabara hii tutaitafutia
suluhisho la kudumu na pindi tukiazna kazi ni lazima tuweke mipango
madhubuti ambayo itaweza kuleta mabadiliko na kupunguza adha ya kero ya
foleni ambayo ilikuwa hapo awali.,”alisema Magufuli.
Dr Magufuli akifafanua zaidi juu
ya suala hilo alisema kwamba katika kupamabana na changamoto hiyo ya
msongamano wa foleni serikali ya wawamu ya nne tayari imeshaanza
jitihada zake za hali na mali ambapo katika kukabilina suala hilo mizani
ya maili moja mabyo ilikuwa ni inachangia kwa kisi kikubwa kuwepo kwa
foleni imeamishia katika eneo la vigwaza.
“Hapa kwanza nilipo wananachi wa
kibaha mmenifurahisha sana kwa kuonyesha upendo wa dhati kwa mapokezi
makubwa ambayo kiukweli nimefarijika lakini kitu kikubwa mabcho
nitakisimamia ni uboreshaji wa miundombinu ya barabara ili zimweze
kupitika na hili nitalivalia njuga kweli kweli nikisaidiana na Koka
ambaye amewza kufanya mabadiliko makubwa katika kipindi chake cha
uongozi hivyo wananchi inapaswa kuhakikisha mnampa kura nyingi yeye,
madiwani pamoja na mimi mwenyewe maana hapa ni kazi tu,”alisisitiza
Magufuli.
Pia alisema kwamba endapo mji wa
kibaha ukiwa barabara nzuri ambazo zinaweza kupitika kwa urahisi bila
ya kuwa kero kutaweza kusaidia kwa kisi kikubwa kupunguza na msongamano
ambao umekuwa ukijitokeza katika jiji la Dar es Salaam, hivyo juhudi
zake zote ni kuuendeleza mji wa Kibaha ambao utaweza kuleta chachu ya
kimaendeleo .
Mgufuli aliwaambia wananchi
anao uzoefu mkubwa katika wizara mbali mbali kwani alishawahi kuwa
waziri wa ujenzi katika kipindi cha miaka 15 hivyo ana imani endapo
akiwa rais atahakikisha katika siku zausoni ataweka mipango kabambe
kwa kujenga barabara nyingine za juu zaidi zaidi ya saba ambazo lengo
lake kubwa ni kuondokana na usumbufu wa msongamano ambao umekuwa ni
kero ya siku nyingi sana.
Akizungumzia kuhusiana na suala
la ardhi Mgufuli alisema kwamba serikali yake itahakikisha kwamba
wananachi ambao wenye maeneo yao atawasimamia kwa hali na mali ili
kuweza kuondokana na migogoro ya ardhi ambayo katika baadhi ya maeneo
inatokana na kugombania maeneo kati ya wananchi na wawekezaji.
Awali Mgombea ubunge wa jimbo la
Kibaha (CCM) Silvestry Koka alimwakikishia Mgombea urais huyo kuwa
atahakikisha changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wa kibaha
mjini atazifanya kazi kwa hali na mali ikiwemo kuhakikisha wanapata
huduma zote muhumi zinasotakiwa ikiwemo, maji, afya, elimu, miundombinu
pamoja na kusimamia kikamilifu suala la wagonjwa wanaofanyiwa vitendo
vya unayanyasaji.
Koka pia aliongeza kuwa katika
kuhakikisha anapambana na janga la umasikini ataviwezesha vikundi mbali
mbali vya ujasiriamali kwa upande wa vijana na wakinamama kwa kuwapatia
mitaji ambayo itaweza kuwasaidia kuachana na kuwa tegemezi , na
kuongeza kuwasaidia wazee ambao wamekuwa wakibaguliwa katika kupatiwa
huduma ya afya.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269