Miili ya makumi waliopoteza maisha wakati wa mashambulizi hayo.
Hali ilivyokuwa eneo la tukiuo.
Ankara, Uturuki
Milipuko
miwili imetokea wakati wa mkutano wa hadhara wenye lengo la maandamano
ya amani katikati mwa Mji Mkuu wa Uturuki, Ankara asubuhi ya leo na
kusababisha vifo vya watu zaidi ya 52 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa
vibaya.
Picha za
televisheni zilionyesha watu waliokuwa na hofu na wengine wakiwa
wamelala chini wakiwa wametapakaa damu miilini mwao. Wakati duru ya pili
ya uchaguzi wa ubunge ikitarajiwa kufanyika mwezi ujao, maandanmano
hayo yalipangwa na vyama vya wafanyakazi wakitaka kumalizika kwa
mashambulizi yanayoendeshwa na serikali dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269