Meneja
Mauzo wa Simu za Tecno, Fred Kadilana akionesha simu aina ya Phanton 5
wakati wa uzinduzi wa tolea jipya la simu hizo uliofanyika Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
Wadau mbalimbli wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Uzinduzi wa simu hiyo toleo jipya ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Meneja
Mauzo wa Simu za Tecno, Fred Kadilana (kulia), akiwagawia zawadi ya
simu hiyo baadhi ya waandishi waliouliza maswali mbalimbali.
Wanahabari wakipokea zawadi ya simu hiyo ya kisasa toleo jiopya.
Na Dotto Mwaibale
MAKAMPUNI
yanayozalisha Simu nchini yameshauriwa kuhakikisha wanakuwa wabunifu
katika kusanifu na kulizasha simu bora ili kwenda sambamba na soko la
dunia.
Wito
huo umetolewa na Meneja mauzo wa simu za Tecno, Fred Kadilana wakati wa
uzinduzi wa tolea jipya la simu ya Phantom 5 uliofanyika Dar es Salaam
juzi.
Kadilana
alisema soko la bidhaa zao linakuwa kwa kasi hususan barani Afrika
hivyo wanafanya jitihada kuhakikisha wanakwenda sambamba na soko la
dunia.
"Soko
la dunia linakuwa kwa kasi na hata bidhaa zetu pia hivyo tunajitahidi
kila kukicha kwenda sambamba na ukuaji wa mahitaji ya wananchi," alisema
Kadilana.
Kwa
upande wake, mkurugenzi wa kampuni hiyo, Daniel Xu alisema falsafa ya
kutengeneza simu bora ni kulenga mahitaji ya soko la dunia.
Alisema
simu ya Phanthom 5 ni toleo linalowapa wateja usanifu wa kipekee wenye
uwezo 32GB katika uhifadhi wa taarifa na pia 3 GB katika mfumo wa kusoma
na kuperuzi katika simu kwa haraka zaidi.
"Simu hii ina uwezo wa 300m Ah katika betri lake hivyo kuondoa usumbufu wa kuchaji simu mara kwa mara," alisema Xu.
Xu alisema kutokana na changamoto za kidunia simu hiyo ina uwezo wa kufurahia mawasiliano katika mazingirq mbalimbali.
Aliongeza
kuwa kwa kuzingatia ubora Tecno imeweza kushinda tuzo ya dunia kwa
ubora na kwa sasa wanaongoza kwa mauzo kwa kipindi cha miaka mitano sasa
barani Afrika.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269