Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M, Baseev Mohamed (kushoto),
akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 20, Mkuu wa Idara
ya Biashara wa benki hiyo, Svikanth T, kwa niaba ya mteja wa benki
hiyo, Jumanne Francis Mchenje wa Tarime mkoani Mara anayeishi jijini
Mwanza aliyejinyakulia kitita hicho cha fedha baada ya kushinda bahati
nasibu ya kwanza inayoendeshwa na benki hiyo kwa ajili ya kuongeza
wateja wapya iliyofanyika Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja Masoko,
Ruheen Kaba.
Bahati nasibu hiyo iliyowashirikisha wateja wa benki hiyo ikichezwa.
Namba iliyoshinda ikihakikiwa. Wa pili kushoto ni Mjumbe kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Jehud Ngolo.
Maofisa wa benki hiyo wakisubiri kuanza kuchezwa kwa baahati nasibu hiyo.
Hapa aliyechaguliwa kuchagua namba akifungwa kitambaa.
Mashine ikichangany'a namba za kushiriki bahati nasibu hiyo.
Bahati nasibu hiyo ikichezwa.
Kitambulisho cha mshindi wa bahati nasibu hiyo, Jumanne Francis Mchenje.
Na Dotto Mwaibale
BENKI
ya I&M Ltd imeanzisha mchezo wa bahati nasibu kwa wateja wapya
wanaojiunga kwenye benki hiyo kwa lengo la kuvutia wataje wao.
Akizungumza
Jijini Dar es Salaam jana Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Baseer
Mohamed alisema shindano la kwanza lilifanyika jana ambapo Jumanne
Francis Mchenje kutoka Tarime mkoa wa Mara aliibuka kuwa mshindi.
Alisema
Jumanne alijishindia Million 20 kwa kufungua akaunti katika benki hiyo
na kuweka kiasi kidogo cha pesa kwenye akaunti yake.
"Jinsi
ya kushiriki bahati nasibu hii ni kufungua akaunti ya benki yetu kisha
kuweka kiasi chochote kwenye akauti yako ndipo tunakuingiza kwenye droo
ya kujishindia million 20,"alisema Mohamed.
Alisema
watakuwa wakifanya mashindano kama hayo kila wiki ili kuonyesha
utamaduni mzuri kwa wataje wao kwani benki hiyo ni makini.
Pia
aliwataka wananchi kufungua akaunti zao katika kipindi hiki cha bahati
nasibu ili kujishindia kitita hicho cha million 20 kila. wiki.
"Benki
hii ni kwa ajili ya Watanzania wote hivyo ni vyema mkajitokeza kwa
wingi kufungua akaunti zenu na kufurahia huduma zinazo tolewa na benki
yetu,"alisema Mohamed.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269