Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah akizungumza
katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa
Mbeya ambapo amesema kuwa Taasisi hiyo imeweza kufanikiwa kupambana na
rushwa kwa kiasi kikubwa ambapo jumla kesi kubwa za rushwa 1,993 kuanzia
mwaka 2004-2015 zimeweza kufunguliwa ambazo ni sawa na ongezeko la
asilimia 81 ikilinganishwa na kesi 384 zilizokuwepo miaka 10 ilioyopita
(1995-2004)
Amesema ,ongezeko hilo la kesi kubwa limetokana na jitihada za
Taasisi hiyo katika kupambana na kuzuia rushwa nchini hasa katika
kipindi cha serikali ya awamu ya nne, chini ya rais Jakaya Kikwete.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akitoa salama za mkoa wa mbeya
katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Takukuru Mkoa wa Mbeya .
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mbeya xavery Mhyella akatoa taarifa ya
Takukuru Mkoa wa Mbeya mbele ya Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo
imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Mkuu Takukuru nchini Dkt, Edward Hosea
Octobar 5 mwaka huu..Picha na Emanuel Madafa ,Jamiimojablog Mbeya
Mkaguzi Mkuu wa Kanda Takukuru Ndugu Joice Shundi akizungumza katika hafla hiyo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Wende wakitoa burudani za ngoma za
asili katika uzinduzi huo wa jengo la ofisi mpya ya Takukuru Mkoa wa
Mbeya .
Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa dini waliohudhuria hafla hiyo ya
uzinduzi wa jengo zilizopo eneo la forest ya zamani karibu na Mahakama
kuu jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269