Katibu
wa Benki ya CRDB, John Rugambo (kulia), akitia saini mkataba huo.
Kutoka kushoto ni Chief Operation Officer wa WHCTZ, Weja Ng'olo, Ofisa
Mtendaji Mkuu wa TMRC, Oscar Mgaya, Mkurugenzi wa Watumishi Housing
Company, Dk.Fred Msemwa na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Charles Kimei.
Hapa hati zikioneshwa kwa wanahabari baada ya kusainiwa.
Mkurugenzi wa Watumishi Housing Company, Dk. Fred Msemwa akizungumza katika mkutano huo.
wadau kutoka benki ya CRDB na Watumishi Housing Company wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
wadau kutoka benki ya CRDB na Watumishi Housing Company wakiwa kwenye mkutano huo. |
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
TAASISI
ya Watumishi Housing Campany (WHC ),imeingia mkataba na Benki ya CRDB
ikiwa ni katika kuwawezesha watu wa hali ya chini kupata mikopo ya
nyumba bora kwa bei nafuu.
Akizungumza
Dar es Salaam leo asubuhi Mkurungezi wa wa taasisi hiyo, Dk.Frank
Msemwa alisema wameamua kuanzisha mikopo ya nyumba za bei nafuu ikiwa ni
mkuinua watu wenye vipato vidogo.
Dk
Msemwa alisema tayari wameshalenga soko la nyumba nchini watajenga
nyumba zenye gharama nafuu ambazo kila mtu ataweza kukopa.
"Zitakuwa ni nyumba bora na kwa gharama nafuu kabisa kila mtu ambaye anakipato ataweza kukopa nyumba hizo," alisema Dk Msemwa.
Alisema
mahitaji ya nyumba nchini ni zaidi ya bilioni 1.9 ambapo kwa jiji la
dar es salaam pekee hitaji la nyumba ni laki nne kwa kila mwaka.
Naye
Mkurugenzi wa CRDB Charles Kimei alisema Dira ya taifa inaangalia
nymba ikiwani kama azina ya kudumu na isiyo haribika huivyo ni vyema
watu wakawekeza kwenye nyumba.
Alisema nyumba nzuri ni matokeo ya watoto wenye uelewa mzuri shuleni kwani hupata sehemu safi kwa kujisomea .
"CRDB
ilikuwa ikikopesha nyumba ila si kwa njia rahisi kama hii inayoanza leo
hivyo watu waje kwa wingi kukopa nyumba ambazo ni bora,"alisema Kimei.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269