Alassane Ouattara
Alassane
Ouattara ameshinda uchaguzi wa urais nchini Ivory Coast kwa wingi wa
kura. Matokeo yalitangazwa kupitia runinga huku rais huyo akishinda kwa
asilimia 83.66.
Hii inamaanisha kwamba hakutakuwa na duru ya pili ya uchaguzi.
Raia wa
Ivory Coast waliamkia habari za ushindi wa Rais Alassane Outtara kama
walivyotarajiwa kwamba rais huyo ataongoza kwa muhula mwengine wa miaka
mitano.
Baada ya
mwongo mmoja wa kutoimarika kwa uchumi na vita vya wenyewe kwa wenyewe,
wengi watafurahia kwamba uchaguzi huo ulifanyika kwa amani.
Uchaguzi wa mwisho wa urais uliofanyika mwaka 2010 ulisababisha vita vya miezi mitano ambapo zaidi ya watu elfu 3000 waliuawa.
Rais wa
zamani Laurent Gbagbo, yuko mjini the Hague katika mahakama ya kimataifa
kuhusu uhalifu wa kivita akingojea kesi inayomkabili.
Ijapokuwa
rais huyo amekosolewa kwa kushindwa kuleta maridhiano na haki,
amesifiwa kwa kuimarisha uchumi wa taifa hilo na kulifanya kuwa taifa
lenye uchumi ulioimarika kama ilivyokuwa miaka ya sabini
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269