Mume wa marehemu akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mke wake
Anneth Christian mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa marehemu Mbezi
Beach - SalaSala Jijini Dar es Salaam na baadae maziko yalifanyika
Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
Mmoja ya wanandugu akitoa heshima ya mwisho.
Mume wa marehemu Anneth Christian akiweka mchanga katika kaburi la mke wake katika Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
Mama wa marehemu akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mwanae
Anneth Christian mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa marehemu Mbezi
Beach - SalaSala Jijini Dar es Salaam na baadae maziko yalifanyika
Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
Mume wa marehemu akiweka shahada la ua katika kaburi la mke wake katika Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
Mtoto wa marehemu akiweka mchanga katika kaburi la mama yake.
Mama wa marehem akiweka mchanga katika kaburi la mwanae.
Wanafamilia wakiweka maua katika kaburi la Anneth Christian.
Mwili wa Marehemu Anneth Christian ukiingizwa nyumbani kwake Mbezi
Beach - SalaSala Jijini Dar es Salaam na baadae maziko yalifanyika
Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
Waombolezaji.
UKATILI WA KIJINSIA SOKO LA TEMEKE WAPUNGUA KWA ASILIMIA 70
Mwezeshaji Sheria katika Soko la
Temeke Sterio, Batuli Mkumbukwa (katikati), akizungumza katika mkutano
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mafanikio waliyopata
ya kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo baada ya
kupatiwa mafunzo na Shirika la Equality for Growth (EfG). Kushoto ni
Mwezeshaji wa Sheria, Christina Simon na Augenia Gwamakombe.
Mkuu wa Mgambo katika soko hilo, Onesmo Osward (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Mfanyabiashara wa matunda katika soko hilo, Isabela Juakali akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Augenia Gwamakombe (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mfanyabiashara wa Soko hilo, Said, Mbonde (kulia), akizungumzia kupungua kwa ukatili wa Kijinsia katika soko hilo.
Wanawake wafanyabiashara katika soko hilo wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
UKATILI wa kijinsia katika Soko la Temeke umepungua kwa asilimia 70 ukilinganisha na miaka mitatu iliyopo imefahamika.
Hayo yalibainishwa na Mwezeshaji wa
Sheria wa soko hilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake katika
soko hilo, Christina Simon wakati akizungumza na waandishi wa habari
waliotembelea soko hilo Dar es Salaam leo asubuhi kujua changamoto za
ukatili wa jinsia katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for
Growth kutoa mafunzo ya namna ya kukabiliana na ukatili huo.
"Hivi sasa vitendo vya ukatili wa
kijinsia katika soko letu umepungua kwa kiasi kikubwa baada ya wanawake
kujitanbua na kupatiwa mafunzi na shirika la EfG" alisema Simon.
Alisema awali matukio ya unyanyasi kila
wiki walikuwa wakiyapokea kati ya matatu na zaidi lakini sasa kwa mwezi
wanaweza kupokea tukio moja au lisiwepo kabisa.
Mwezeshaji wa Sheria, Taus Ali, alisema
katika soko hilo kulikuwa na unyanyasaji mwingi, lugha za matusi ambazo
likuwa zimekithiri lakini hivi sasa hali hiyo haipo na kama ipo ni kwa
kiwango kidogo hasa baada ya kuletewa mradi wa Mpe Riziki si Matusi na
EfG.
Mfanyabiashara, Said Mbonde alisema hivi
sasa unyanyasaji wa kijinsia kwenye soko hilo haupo kwani hapo awali
kulikuwa na tabaka la kufanyabiashara kwani biashara aliyokuwa
wanaifanya wanaume walikuwa hawaruhusiw kufanya wanawake lakini sasa
kila mmoja wao anafanyabiashara hizo zikiwemo za udalali.
Mfanyabiashara wa matunda katika soko
hilo, Isabela Juakali alisema tabia iliyokuwepo zamani ya mgambo
kuwamwagia biashara zao wafanyabiashara ndogo ndogo hivi sasa haipo
kabisa baada ya kuelewa na kufuata kanuni na maelezkezo ya utendaji
kazi.
Mkuu wa Mgambo katika soko hilo, Onesmo
Osward alisema siku hizi malalamiko ya mtu kutukanwa au kupigwa hayapo
kabisa jambo lililoongeza utulivu na amani katika soko hilo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269