Miongoni
mwa nyumba zilizopo Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Ilemela Mkoani
Mwanza ambazo huathirika na kero ya Maji kuingia ndani pindi mvua
zinapoanza kunyesha.
Pichani
ni mmoja wa wakazi wa Kilimahewa akitoa maji ndani ya nyumba yake
kutokana na mvua iliyoanza kunyesha majira ya saa kumi na mbili alfajiri
hii leo. Hadi tunaenda hewani (saa 10:30 asubuhi) Mvua hiyo inaendelea
kumiminika mdogomdogo.
Picha na Loyce Nhaluke
Mbali
na Kilimahewa, Pia wakazi wa Mabatini Jijini Mwanza hukumbwa na kero ya
Mafuriko wakati wa Mafuriko na kwa miaka mingi juhudi za kuwahamisha
zimekuwa zikigonga mwamba linapokuja suala la kuwatafutia makazi mapya.
Mara kadhaa mafuriko katika maeneo hayo yamekuwa yakisababisha athari mbalimbali ikiwemo vifo.
Maji hadi ndani, hakika ni hatari
Maji yakitolewa ndani
Kilimahewa Manispaa ya Ilemela
Mvua
kubwa iliyonyesha katika Jiji la Mwanza na vitongoji vyake imenyesha
mvua kubwa sana tangu saa 1:15 Asubuhi leo mpaka saa 4:15mvua
iliyosababisha Barabarani za Jiji kujaa maji yaliyopelekea daraja moja
lililopo Mabatini Barabara ya Nyerere kutopitika Gari.(NA RIPOTA WETU
UJIJIRAHAA BLOG MWANZA)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269