Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) Doreen
Sinare akielezea umuhimu wa wanamuziki kujisajili kwao kupitia Kampuni
iliyopewa jukumu la kuendesha zoezi usajili, Copyrights Management East
Africa Limited (CMEA) ilikuweza kupata haki zao kutokana na kazi zao.
Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni ya CMEA, Abdi Zagar akielezea jinsi ya
mfumo wa kisasa wa ukusanyaji taarifa za wanamuziki kwenye vituo vya
televisheni na redio kwa ajili ya kutumiwa na Cosota ili kufanya malipo
sahihi kwa wanamuziki na wadau wake.
Mwanamuziki, Barnaba akitoa maada katika semina hiyo iliyoandaliwa na
Cosota na CMEA kwa ajili ya kuwapa elimu wanamuziki na wadau wake
kuhusiana na malipo ya mirahaba.
Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akijibu moja
ya maswali katika semina hiyo. Mutahaba aliwahamasisha wanamuziki
kujisajili CMEA kwa lengo la kupata haki kutokana na kazi zao.
Wanamuziki wa muziki wa dansi, Chalz Baba na Jonico Flower wakifuatilia
semina hiyo ambayo iliwapa somo kuhusiana na umuhimu wa kujisajili
kupitia kampuni ya CMEA na Cosota ili kufaidika na kazi zao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse akifafanua jambo kuhusiana
na faida za wanamuziki na wadau wake mara baada ya kujisajili na kuanza
kulipwa fedha zao.
Chama
cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) kwa kushirikiana na kampuni ya
kusimamia kazi za wanamuziki nchini Copyrights Management East Africa
Limited (CMEA) wataanza kulipa mirabaha ya wanamuziki na wadau wake
kuanzia mwakani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Cosota, Doreen Sinare alisema kuwa wanamuziki, watunzi na ma’producer’ watalipwa asilimia 60 kwa kila wimbo au video itakayochezwa katika redio na televisheni yoyote ndani na nje ya nchi kwa kutumia vifaa bora vilivyowekwa na kampuni ya CMEA.
Doreen alisema kuwa manamuziki, msanii alitakiwa kupata asilimia 70 ya kazi yake, lakini asimilia 10 itakatwa katika malipo hayo na kuingia katika mifuko ya jamii kwa mahitaji yake ya baadaye.
Alisema kuwa wanamuziki ni sawa na wafanyakazi wengine na asilimia 10 hiyo itamwezesha kujipatia kipato chake kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine katika taasisi mbalimbali.
Kwa mujibu wa Sinare alisema kuwa ili kuhakikisha kila mwanamuziki anafaidika na kazi yake, watashirikiana na vyama vingine vya Hakimiliki katika nchi mbali mbali kwa kutumia hati ya malipo zinazotokana na bei za matangazo kwa televisheni na vituo vya redio.
Alisema kuwa Cosota na CMEA pia watawapa ushirikiano vyama hivyo ili nao waweze kupata haki za malipo ya wanamuziki wao kwa vituo vya televisheni na redio vitakavyotumia kazi za wanamuziki wa nje.
“Lengo la Cosota na CMEA ni kuona wasanii wanafaidika na kazi zao, mirabaha ya kwanza tutaanza kulipa Januari 2 na kwa sasa tupo katika hatua za mwisho kukamilisha jinsi tutavyolipa, ndiyo maana tumetoa semina kwa wanamuziki, lengo ni kuwahamasisha kujisajili,” alisema Sinare.
Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse alisema kuwa mbali ya wanamuziki, kampuni yao itawawezeha pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.
Matthysse alisema kuwa kampuni yao imewekeza mitambo ya kisasa inayowezesha kuchapisha na kuhakiki nyimbo pindi zinapochezwa hewani na televisheni na redio na kutoa ripoti za aina mbalimbali zinazohitajika kutumika kwa malengo maalum.

“Pia
tunapokea na kuhifadhi nyimbo kwenye mitambo maalum kwa matumizi ya
uhakiki, na kudhibiti kiasi cha mirabaha ambacho Cosota kupitia vyombo
vya habari inatakiwa kuwalipa wasanii kulingana na idadi kamili ya
urushwaji wa kazi zao,” alisema Matthysse.
Alisema kuwa wanamuziki na wasanii wengine ambao hawatakuwa na usajili, watakosa haki zao pamoja na CMEA kuendelea kurekodi kazi zao zinazochezwa katika redio na televisheni mbali mbali. “Ni muhimu kwao kujisajili, kutojisajili ni kupoteza haki zao zinazotokana na kazi yako,” alisisitiza.

No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269