Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake aliombatana nao Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto) kabla ya kuelekea kambi ya Nyarugusu walipita ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita kumsalimia pamoja na kusaini kitabu cha wageni. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
JUMUIYA ya Kimataifa imekumbushwa kuisaidia Tanzania katika kuhudumia wakimbizi kutoka Burundi na Kongo ambao wanaishi katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kukamilisha ziara yake mkoani Kigoma.
Alisema kwamba serikali ya Tanzania kwa miaka mingi imekuwa na moyo wa huruma wa kusaidia majirani zake kwa kuhifadhi wakimbizi na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuona hilo na kusaidia Tanzania kufanikisha hifadhi ya wakimbizi.
Alisema Umoja wa Mataifa umekuwa ukishuhudia namna ambavyo serikali ya Tanzania inahudumia wakimbizi na kuridhika na hata pale ilipowapatia haki za kuwa Watanzania kwa kuwapa uraia na pia kusaidia kuwarejesha makwao wakati hali ilipokuwa njema.
Hata hivyo amesema kwa sasa hali ya Burundi na Kongo si njema na hivyo Watanzania kupata tena kazi yakuhifadhi wakimbizi.
Alisema Tanzania kwa huruma yake imetoa ardhi zaidi ili kupunguza msongamano katika kambi ya Nyarugusu na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kusaidia kukamilisha makazi hayo mapema kabla ya mvua za masika ili wananchi hao waweze kuishi kwa amani.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akimsikiliza kwa makini Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuelekea kambi ya Wakimbizi Nyarugusu.
Alisema kambi ya Nyarugusu ni ya tatu kwa ukubwa duniani na inahifadhi zaidi ya wakimbizi 150,000 wakiwemo watoto na wanawake na wanahitaji huduma za shule, afya, maji na mengine.
Aidha wanahitaji nishati na hali hiyo haiwezi kuwezeshwa na serikali ya Tanzania pekee kwani watakuwa wakielemewa na huruma yake na moyo wa upendo kwa majirani zake.
“Dunia ikumbuke wema wa watanzania kwa miaka yote hii, na isaidie kuweka sawa hali ya kambi hiyo ili huduma zote muhimu za wananchi zipatikane” alisema mratibu huyo.
Akizungumza kuhusu wajibu wa Umoja wa Mataifa, alisema mashirika yake yamekuwa yakishirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba wanatoa huduma kwa wakimbizi hao na kutaka wadau duniani kusaidia mashirika hayo na serikali ya Tanzania kufanikisha mahitaji muhimu kwa wakimbizi hao hadi hali itakapokuwa shwari katika nchi zao na kurejea kuishi makwao.(P.T)
Tanzania
imetoa maeneo matatu zaidi ya kupunguza msongamano katika kambi ya
Nyarugusu na maeneo hayo yanahitaji huduma za msingi kama barabara,
maji, vituo vya afya na shule.
Katika
ziara hiyo ambayo aliambatana na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Maulidah Hassan, pamoja na kukagua maendeleo ya kambi ya
Nyarugusu pia walikagua miradi inayofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani
ILO na ile ya Shirika la Mpango wa idadi watu duniani UNFPA.
ILO
Kigoma inaendesha mafunzo ya ujasirimali kwa vijana kwa lengo la
kuwawezesha kujiajiri wenyewe na kuhudumia familia zao kwa kuziwezesha
kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao.
Katika
msafara huo walikuwepo maafisa kutoka Shirika la linalohudumia Wakimbizi
(UNHCR) ofisi ya Kasulu mkoani Kigoma (walioipa mgongo kamera).
Alisema
kwamba amefurahishwa na mradi huo ambao unawawezesha vijana kutambua
fursa mbalimbali zilizopo na kuzitumia vyema kufanikisha maendeleo ya
familia zao.
“Naona
uwezekano wa vijana hawa kujiajiri na kuziwezesha familia zao kuondokana
na tatizo la kipato.. elimu hii inaweza kutanzua mambo mengi na kuondoa
changamoto nyingine zinazoambatana na kukosa kipato” alisema mratibu
huyo.
Mkoa wa
Kigoma una mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa yakifanya kazi mbalimbali
za maendeleo na za kutoa huduma za kibinadamu kwa wakimbizi.
Mashirika
hayo ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza miradi mbalimbali mkoani Kigoma
ni pamoja na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Shirika la Afya
Duniani ( WHO), Shirika la Mpango wa Uzazi (UNFPA), Shirika la Kazi la
Kimataifa ( ILO), Shirika la Kuhudumia Watoto ( UNICEF), Shirika la
Kuhudumia Wahamiaji ( IOM), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)
na Shirika la maendeleo (UNDP).
Akizungumza
Afisa anayeshughulikia Ustawi na Usalama UNHCR, Kasulu, Bi. Zenobia
Mushi, alisema shirika lake litaendelea kushirikiana na serikali ya
Tanzania na ya mkoa wa Kigoma katika kuhudumia wakimbizi kwa kuhakikisha
kwamba mahitaji yao ya msingi yanapatikana.
Naye
Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya alishukuru
Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuwa tayari kusaidia mkoa wake.
“
Tunashukuru kwa mambo yanayofanywa na Umoja wa Mataifa katika dhima
nzima ya ushirikiano katika kuhakikisha kwamba pengo la maskini na
matajiri linazibwa na umaskini unaondolewa katika mkoa wa Kigoma.”
Ofisa wa
Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akipiga picha
kwenye bango linaloonyesha Serikali zinazofadhili misaada kwa Wakimbizi
nchini Tanzania lililopo katika ofisi za UNHCR Kasulu.
Naye Mkuu
wa wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akizungumza kuhusu hali ya kambi
ya Nyarugusu alisema kwamba hali ya kambi si nzuri na wakati msimu wa
masika ukikaribia ni vyema Jumuiya ya Kimataifa ikaharakisha kukamilisha
miundombinu ili kupunguza msongamano Nyarugusu.
Serikali
imetoa maeneo mengine ya Nduta yaliyoko Kibondo na na Ntendeli, Kakonko
kwa ajili ya kupunguza uwingi wa watu katika kambi hiyo.
DC huyo
pia alisema kwamba kuna uharibifu mkubwa wa mazingira na lazima wadau
wote washirikiane kuhakikisha kwamba mazingira yanaboreshwa pamoja na
kupokea wakimbizi na kuwapa makazi.
Alisema kambi hiyo ilipangwa kuwa na watu elfu 50 kwa miaka ya 1996 lakini sasa inaweka wakimbizi wengi zaidi.
Aidha
alisema kwamba pamoja na kupokea wakimbizi hao, inaonekana baadhi yao
wameingia kufanya uhalifu na kuomba wakimbizi kushirikiana na polisi
kuwataja wahalifu hao ili wadhibitiwe.
Kuwepo
kwa kundi kubwa la wakimbizi kunasababisha uharibifu wa mazingira kama
inavyoonekana pichani wakimbizi wakitoka kukata kuni kwenye misitu
iliyopo karibu na kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Aidha
katika mazungumzo ya shukurani kwa namna serikali ya Kigoma inavyotoa
ushirikiano kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika miradi ya maendeleo
na misaada kwa wananchi na kwa wakimbizi, Mwakilishi wa Shirika la
mpango wa idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem alisema
kwamba kumekuwepo na mafanikio mengi kutokana na ushirikiano huo.
Alisema
anachokiona yeye anaona hali ya baadae ya taifa la Tanzania kuwa bora
zaidi kutokana na kuwapo kwa ushirikiano mzuri kati ya serikali,
mashirika ya umma na kundi kubwa la vijana ambalo kwa sasa linapokea
elimu mbalimbali kwa manufaa yao na ya baadae.
“Taifa la
Tanzania nusu yake ni vijana na sehemu kubwa ni chini yake, taifa hili
lina hali njema kabisa ya siku za usoni kutokana na ushirikiano wenye
lengo la kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na wengi” alisema Kanem.
Anasema
kwa kuangalia program zilizopo zinazotekelezwa kwa pamoja na mashirika
ya Umoja wa Mataifa na serikali anaona mafanikio ya mafunzo ya
ujasiriamali na pia elimu inayotolewa kwa watu kwa malengo ya
kufanikisha maendeleo.
Alisema
UNFPA imefurahishwa sana namna mafunzo yanavyoendeshwa kwa vijana
mafunzo ambayo yanaleta mshikamano wa pekee katika kufanikisha ustawi wa
jamii na taifa kwa jumla.
Aidha
alifurahi kuona kwamba wanawake wanashiriki katika kutoa elimu hivyo
kuingiza sauti katika mafanikio ya jamii na uongezaji wa uelewa miongoni
mwa jamii.
Mratibu
huyo Mkazi wa UN Tanzania, Alvaro Rodriguez na timu yake wamerejea Dar
es Salaam baada ya ziara ndefu kuangalia miradi ya Umoja wa Mataifa
inavyoleta tija na ufanisi wa maisha katika jamii.
Mratibu huyo alitembelea mikoa ya Manyara, Singida, Tabora na Kigoma.
Katika
ziara yake alioneshwa kufurahishwa na miradi hiyo inavyobadili jamii
husika na kusema kwamba umoja huo utaendelea kufadhili miradi ya
maendeleo nchini Tanzania.
Mkuu wa
Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (kulia) akielezea changamoto
mbalimbali zinazowakabili kambini hapo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake aliombatana nao Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa wa
Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto)
kabla ya kutembelea makazi ya wakimbizi hao.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (kulia) na Ofisa wa Mambo ya Nje
kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan wakirekodi mambo muhimu
wakati wa kupokea taarifa ya maendeleo ya kambi ya Wakimbizi ya
Nyarugusu kutoka kwa Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile
(hayupo pichani).
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akizungumza jambo kwenye mkutano wa
kupokea taarifa ya kambi hiyo.
Kutoka
kushoto ni Afisa mahusiano wa UNHCR, Ofisi ya Kasulu, Agnes Mwangoka,
Mshauri na Mtaalum wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Hoyce
Temu, Mwandishi wa Habari, Prosper Kwigize pamoja na Ofisa wa Mambo ya
Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan wakielekea kwenye kambi
za Wakimbizi baada ya kupokea taarifa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini,
Dkt. Natalia Kanem wakikagua ndani ya mahema wanakoishi Wakimbizi wapya
wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini,
Dkt. Natalia Kanem wakiuliza jambo kwa Ofisa Mtafiti Mshirikishi wa
ofisi za UNHCR, Kasulu, Mariam Khokhar walipotembelea ndani ya mahema
wanakoishi Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya
Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Wa pili kushoto ni Mkuu
wa Kambi ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile.
Eneo la mahema ya kulalia familia za Wakimbizi wapya wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu.
Mmoja wa Wakimbizi akiwa na mwanae nje ya chumba chake na mwanae katika kambi ya Nyarugusu.
Kuni zikitumika kupikia chungu cha Maharage kambini hapo.
Mtoto
ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akikoleza moto
ulioonekana kufifia wakati akijiandalia chakula chake cha mchana kama
alivyonaswa na kamera yetu.
Moja ya
familia ya Wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu wakiangalia msafara wa
Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini uliotembelea kambini hapo
mwishoni mwa juma.
Ofisa wa
Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akipozi na
moja ya familia katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Rais wa kambi ya
Wakimbizi ya Nyarugusu, Bi. Abilola Angelique wakati wa ziara yake ya
kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269