Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti
wa mambo ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa Professa Nigel Lightfoot
akitoa mada kwa wadau mbalimbali wa afya kutoka katika mashirika na
taasisi mbalimbali za Afrika na Ulaya zinazoshughulikia masuala ya afya
katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia
bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola na mengineyo katika
bara la Afrika na kwingineko duniani.
Dokta Julius Julian Lutwan kutoka
Uganda akitoa mada kwa wadau mbalimbali wa afya kutoka katika mashirika
na taasisi mbalimbali za Afrika na Ulaya zinazoshughulikia masuala ya
afya katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili
njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola na mengineyo
katika bara la Afrika na kwingineko duniani.
…………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
NCHI za kiafrika zimetakiwa kuweka
nguvu ya pamoja kuhakikisha zinapata njia bora na za kudumu za
kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola na kuachana na utegemezi wa
misaada kutoka nchi wahisani.
Dokta Andrew Kitua wa taasisi ya
afya ya Ngalakeri ya Morogoro aliyasema hayo jana katika warsha ya siku
mbili ya kujadili njia bora na za kudumu za kupambana na magonjwa ya
mlipuko kama Ebola inayofanyika mkoani Arusha.
Alisema kwakuwa bara la afrika ni
miongoni mwa waathirika wa magonjwa hayo wadau husika katika sekta ya
afya kwa pamoja na serikali za nchi husika hazina budi kuwekeza nguvu
katika kutafuta suluhisho la magonjwa hayo.
Alisema ingawa tayari kuna
jitihada mbalimbali zinafanyika katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo
lakini bado kumeonekana kuna changamoto kubwa ya kukabiliana nayo katika
maeneo yanayoathirika.
“Waafrika tunahitajika kuweka
nguvu ya pamoja katika kuhakikisha tunapata njia bora na za kudumu za
kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola,”
“Warsha yetu ya siku mbili
inayoshirikisha wadau kutoka mashirika na taasisi mbalimbali za afya
itajadili na kubadilishana uzoefu wa jinsi ya kupambana na magonjwa hayo
na hatimaye kupata mikakati maalumu ya kuiwekea nguvu dhidi ya
mapambano hayo,” alisema Dokta Kitua.
Kwa upande wake Professa Julias
Lutwan kutoka Uganda alisema nchi zote kwa pamoja bila kujali kama
zimewahi kuathirika au la zinahitajika kujiweka tayari kukabiliana na
magonjwa hayo.
Alsema kwa afrika ukanda wa nchi
za magharibi zinaonekana kupata athari hiyo kwa kiasi kikubwa
unapolinganisha na ukanda wa mashiriki lakini bado kwa pamoja
tunahitajika kujiweka sawa kwa tahadhari katika hilo.
Kwa upande wa changamoto
wanazokabiliana nazo katika tafiti wanazofanya kwa pamoja na mapambano
ya jumla ya magonjwa hayo alisema mawasiliano na kada za chini katika
maeneo ya vijijini ni miongoni mwa changamoto kubwa.
Alisema kwa kuwatumia wataalamu
mbalimbali wa mawasilino wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kurahisisha
lugha ya mawasiliano ili jamii ya chini iweze kupata ufahamu wa jinsi ya
kupambana na magonjwa husika.
Warsha hii inayoshirikisha
wadau mbalimbali wa sekta ya afya kutoka barani afrika na ulaya
imeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na
kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269