Waziri wa
Fedha wa Ufaransa Michel Sapin (kushoto) na mkurugenzi mkuu wa IMF,
Christine Lagarde, Mei 28, 2015 katika mji wa Dresden, Ujerumani.
Na RFI
Mkurugenzi
mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Christine Lagarde, anaweza
kusalia kwenye wadhifa wake kwa sababu "hana hatia", Waziri wa Fedha wa
Ufaransa, Michel Sapin, amesema Alhamisi hii katika mkutano na waandishi
wa habari mjini New York.
Lagarde
ametumwa mbele ya mahakama ya Ufaransa kwa madai ya kuhusika kwake
katika kesi ya Mkopo kwa Bernard Tapie wakati alikuwa Waziri wa Uchumi
nchini Ufaransa.
"Lagarde hana hatia, kwa hiyo sioni jinsi gani hali hii inaweza kumzuia kuendelea na majukumu yake ya sasa", Sapin amesema.
Waziri wa
Fedha wa Ufaransa alikuwa mjini New York katika mkutano wa mawaziri wa
nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya ufadhili
wa kundi la Islamic State.
"Sheria
ya Ufaransa inaundwa kwa kanuni ya msingi kabisa, ambayo ni ile ya mtu
kutokua na hatia kabla hajahukumiwa", Michel Sapin ameonya. "Christine
Lagarde ananufaika na sheria hiyo".
"Hakuna
sababu leo ya kubadili jambo lolote katika utendaji kazi wa majukumu
yake. Ufaransa kama mwanachama wa bodi ya uongozi ya IMF inaamini kwamba
Lagarde bado ana uwezo kamili wa kuendelea kutekeleza majukumu yake",
amesema Waziri wa Fedha wa Ufaransa.
Alipoulizwa
kama Ufaransa imepoteza nafasi kwenye uongozi wa IMF kwa sababu ya
jambo hili, Michel Sapin amekumbusha kwamba "taasisi za IMF zitarejelewa
upya. Ni katika wakati huo ambapo swali hilo litajitokeza", ameongeza
Sapin.
Michel
Sapin amekataa kutoa maoni yake kwa undani kuhusu uamuzi wa Mahakama ya
Jamhuri (CJR). Mahakama hii, amesema, "inafanya kazi yake, inafanya
hivyo hadi mwisho na itafanya hivyo hadi mwisho bila maoni yoyote kutoka
kwa mjumbe hata mmoja wa Serikali ya Ufaransa kuhusu kazi hii."
Kwa
mujibu wa chanzo cha mahakama, CJR imeamuru kwamba Bi Lagarde
atahukumiwa kwa uzembe katika usimamizi wa fedha za umma, kosa ambalo
alifanyiwa uchunguzi katika majira ya joto mwaka 2014.
Kesi
ilianza 2008 wakati Mahakama binafsi ya usuluhishi ilipitishwa na Wizara
ya Uchumi, wakati huo ikiongozwa na Bi Lagarde, ilimpa Bernard tapie
zaidi ya Euro milioni 404.
Bernard Tapie alikua akibaini kwamba akifanyiwa utapeli na benki ya Mkopo ya Lyon wakati mauzo ya kampuni ya Adidas mwaka 1994.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269