Seehmu ya magari yakiwa kwenye bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni
Na K-Vis Media/Khalfan Said
WAFANYAKAZI
Saba wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, TPA, Bandari ya Dar es Salaam, wametiwa
mbaroni na polisi huku wengine wanane wakitoroka wakituhumiwa kula njama za
kuikosesha serikali mapato yatokanayo na kodi na ushuru mwingine, baada ya
kubainika upotevu wa makontena elfu 11, 884, na magari 2019.
Waliotiwa
mbaroni hadi kufukia asubuhi ya leo Desemba 29, 2015 ni pamoja na John Elisante, Leticia Masaro,Christina
Temu, Marina Chawala,Adnan Ally,Msoud Selemani na Benadeta Sangawe.
Waliotoroka
na wanasakwa na polisi ni pamoja na Happy Naftal,Nathan Edward, Aron Lusingu,
Amani Kazumari, John Mushi, Valentine Sangawe, Bonaseet Kimaina na Zainab
Bwijo.
Upotevu
huo umetokea kwenye bandari kavu 7 tofauti ikiwemo ile ya kampuni kubwa hapa
nchini, AZAM, ambayo kwa mara nyingine tena imejikuta inaingia kwenye kashfa ya
kukwepa kodi baada ya kubainika kuwa makontena 779 kati ya makontena hayo
yaliyotajwa hapo juu yalipita bandari ya Dar es Salaam bila kulipiwa ushuru.
Kashfa
hiyo imegundulika kufuatia ziara ya kushtukiza aliyofanya Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi, na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa mara tu baada ya kuapishwa na
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, kushika wadhifa huo.
Waziri
Mbarawa amesema pia jumla ya magari 2,019 nayo yameingia nchini bila ya
kulipiwa ushuru.
Profesa
Mbarawa amesema, kashfa hiyo mpya imebainika baada ya Waziri Mkuu, Mh. Kassim
Majaliwa kuagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania, TPA kwa kushirikiana na vyombo
vingine wafanye uchunguzi wa kina ili kubaini hujuma dhidi ya mapato ya taifa
pale bandarini.
Kufuatia
uchunguzi huo, Profesa Mbarawa amesema, makontena na magari hayo baada ya
kupitishwa bandarini na kupelekwa kwenye bandari kavu 7 tofauti ndipo
yalipoyeyuka yakiacha upotevu wa kodi jumla ya shilingi za Kitanzania Bilioni
49.
Aliyataja
makampuni yanayomiliki bandari hizo kavu kuwa ni pamoja na Azam, ambapo
makontena 779, bandari kavu ya TRH 4,424, JEFAG, 1450), AMI, 4,384.
Makampuni
mengine ni MOFED makontena 61 na kampuni ya DICD 491,
Waziri
Mbarawa amesema baada ya kubaini upotevu hadi kufikia leo Desemba 29
mwaka huu watumishi 7 kati ya 15 waliokuwa wamehusika na ukusanyaji wa mapato
ya Wharfage katika ICD na CFS wamekamatwa na kufikishwa polisi ili waweze
kuchukuliwa hatua za kisheria huku wengine wanane wakiwa wametoroka na polisi
imeanza kuwasaka.
Waziri
Mbarawa ametoa siku 7 makapuni ya uwakala 243 yaliohusika na upotevu huo wawe
wamelipa kodi hizo.
Bandari ya Dar es Salaam, ambayo bado inakumbwa na msuko suko wa uvushaji mizigo bla kulipa kodi
Waziri Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, (wapili kulia), wakati wa ziara yake ya kushtukiza pale bandarini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269