Mbunge wa
Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Bonnah Kalua
akizungumza na vyombo vya habari.(Picha na Maktaba).
Na Skolastika Tweneshe-MAELEZO
Mbunge wa
Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Bonnah Kalua
amesema kuwa hakuna nyumba ya mwananchi itakayobomolewa ambayo imejengwa
katika umbali unaohitaji kisheria wa mita 60 kutoka mtoni.
Mh.Kalua alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wananchi wa Karakata kwenye mkutano wa hadhara.
Aidha
alitoa wito kwa wale ambao wamejenga ndani ya mita 60 na nyumba zao
zimewekewa X kujiorodhesha majina yao kwa wenyeviti wa mitaa ili
wamfikishiea Ofisi kwake kwa ajili ya kulifuatilia jambo hilo kwa
ukaribu na hatimaye wapate haki zao.
Mh.Bonna
aliwatahadharisha wananchi kutodanganywa na watu wanaowachangisha fedha
kwa kigezo cha kufungua kesi mahakamani kuwa ni uongo na hawana nia
nzuri kwa wananchi kwa sababu kesi ya bomoa bomoa tayari ilishafunguliwa
kwa niaba ya nchi nzima.
Aliwataka wananchi kuwa wavumilivu mpaka hapo shauri lilipo mahakamani litakapotolewa tamko
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269