Mtaalamu
wa Matairi kutoka Kampuni ya TBL Group, Peter Muthee, akiwalezea
Maofisa wakaguzi wa Jeshi la Polisi Kikosi Usalama Barabarani jinsi ya
kutambua matairi yaliyo na athari za kiusalama wakati wa mafunzo
maalumu kwa maofisa hao yaliyofanyika jijini Dar es Salam mwishoni mwa
wiki.
-Yametolewa na kampuni ya TBL Group
Maofisa
wa polisi kutoka kitengo cha usalama barabarani wakibadilishana mawazo
na mtaalamu wa matairi kutoka TBL wakati mafunzo maalumu kwa maofisa hao
yaliyofanyika jijini Dar es Salam mwishoni mwa wiki.(P.T)
Mkufunzi
wa madereva kutoka Kampuni ya Bia TBL, Hubert Kubo akizungumza na
Maofisa Wakaguzi wa Jeshi la Polisi Kikosi Usalama Barabarani wakati wa
mafunzo maalumu kwa maofisa hao yaliyofanyika jijini Dar es Salam
mwishoni mwa wiki.
Afisa wa
polisi Kikosi Usalama Barabarani Smax Ibrahim akitoa mada juu ya usalama
wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salam mwishoni mwa
wiki.
Mkurugenzi wa Mafunzo wa TBL Group,Gaspar Tesha akitoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Katika
mafunzo hayo yatakayofanyika mikoa mbalimbali polisi pia walishiriki
zoezi la kufundisha zoezi la ukaguzi wa magari kama wanavyoonekana
wakiangalia mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo akikagua gari.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269