Na
Mwandishi Maalum, New York
Mwenyekiti wa Jopo la Ngazi ya juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Kiafya, Rais Mstaafu, Mhe. Jakaya
Mrisho Kikwete, jana Jumatatu, amemkabidhi Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban ki Moon,
Ripoti ya Jopo lake.
Mhe. Jakaya Kikwete aliteuliwa na Ban Ki Moon, kuongoza Jopo lililokuwa na wajumbe watano
mwezi Aprili 2015. kwa mujibu
wa hadidu za rejea Jopo hili lilitakiwa kutekeleza majukumu yake kuanzia mwezi Mei hadi Desemba 2015.
Akipokea ripoti
hiyo, katika hafla fupi
iliyofanyika Ofisini kwa Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa . Ban
Ki Moon, pamoja na kumshukuru Mwenyekiti wa Jopo Mhe. Jakaya
Kikwete pamoja na timu yake,
amesisitiza kwamba, mapendezo yaliyotolewa na Jopo hilo
yatazingatiwa na kufanyiwa kazi.
“ Ninatoa shukrani zangu za pekee na za dhati kwako
wewe kama Mwenyekiti kwa uongozi wako , na pia kuwashukuru wajumbe uliofanya
nao kazi. Ripoti hii ambayo imesheheni mapendekezo
na ushauri itazingatiwa na kufanyiwa
kazi”. Amesema Ban Ki Moon
Akabanisha kwamba,
mapendekeo na ushauri uliomo
ndani ya Ripoti ya Jopo atauwasilisha pia kwa Shirika la Afya Duniani ( WHO).
Katibu Mkuu pia amesema Ripoti hiyo itasaidia sana
katika kutoa mwongozo kwa Jumuiya ya Kimataifa juu ya namna ya kuimarisha na kuboresha
miundombinu ya afya ili iweze kukabiliana na magonjwa ya milipuko.
Vile vile Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa amemhakikishia Mwenyekiti wa Jopo Mhe. Jakaya Kikwete na wajumbe wake
kwamba, Ripoti hiyo itawekwa hadharani mapema iwezekanavyo ili Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na makundi mbalimbali ya jamii waweze
kuisoma.
Kwa upande wake, Mwenyekiti
wa Jopo, Rais Mstaafu Mhe. Jakaya
Mrisho Kikwete, amemshukuru
Katibu Mkuu Ban Ki Moon, kwa kumpatia heshima ya kuongoza Jopo hilo, jopo ambalo amesema walifanya kazi
kwa ushirikiano wa hali ya juu.
Wajumbe wengine
wa Jopo hilo walikuwa ni
Bw. Celso Amorim ( Brazil),
Micheline Calmy ( Switzerland), Marty Natalegawa ( Indonesia) Joy Phumapi ( Botswana) na Rajav Shah ( USA).
Jukumu kubwa ya
jopo hilo kwa mujibu wa hadidu za
rejea, pamoja na mambo mengine, lilikuwa
ni kutoa mapendekezo ya namna
ya kuimarisha mifumo ya kitaifa na kimataifa katika kuzuia na kukabiliana na majanga ya kiafya yakiwamo magonjwa ya mlipuko, ikiwa ni pamoja na kujifunza
kuhusu mwitikio wa Jumuiya ya
Kimataifa kufuatia kuibuka kwa janga la ugonjwa wa Ebola.
Katika utekelezaji wa
majukumu yake Jopo lilikutana
na kufanya majadiliano ya kina na makundi mbalimbali yakiwamo ya wataalamu,
wawakilishi wa nchi tatu
ambazo ziliathirika sana na ugonjwa wa
Ebola ( Liberia, Siera Leone na Guinea),Mashirika ya Kimataifa
na Kikanda , Taasisi za Fedha za kimataifa, wahudumu wa Afya, Wasomi ,
Watafiti, Sekta Binafsi na wataalam
wa fani
na kada mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269