Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga,
akisaini kitabu cha Wageni baada ya kuwasili Chuo cha Bahari Dar es
Salaam (DMI), wakati wa Mahafali ya Chuo hicho. Anayeshuhudia ni Mkuu wa
Chuo hicho Profesa Yasini Songoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga,
akipata maelezo kutoka kwa Mhandishi wa Meli Stephen Mziray kuhusu
utendaji kazi wa mashine mbalimbali za kuongozea Meli.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga,
akionyeshwa Mitambo mipya katika chumba maalum cha kuongozea Meli kutoka
kwa Eng. Deizm Mley.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, (wa
nne kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa
chuo hicho pamoja na baadhi ya wahitimu.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga,
akizungumza na wahitimu (hawapo pichani) katika mahafali ya chuo hicho
yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga,
akimtunuku cheti mmoja kati ya wanafunzi bora waliofanya vizuri katika
masomo yao Chuoni hapo.
…………………………………………………………………………………….
Wahitimu wa kozi mbalimbali wa
Chuo cha Bahari, Dar es Salaam (DMI), wametakiwa kufuata weredi na
kufanya kazi kwa bidii ili kukuza uchumi wa nchi ili kufikia lengo la
kustawisha pato la kati ifikapo mwaka 2025.
Pia wametakiwa kuzingatia sheria
na kanuni za kazi kitaifa na kimataifa sanjari na kuwa waadilifu ili
wasiwe majibu na waendane na kasi ya Rais wa awamu ya tano Dk. John
Mafuguli katika utendaji kazi na kuwa na uzalendo kwa taifa kwa
kutanguliza maslahi ya nchi mbele.
Wahitimu hao pia wametakiwa kujiendeleza kitaaluma ili kuendana
na kasi ya mahitaji ya dunia ya sasa kwa lengo la kupambana na soko la
ajira kulingana na vigezo vinavyohitajika kitaifa na kimataifa.
Hayo yalizungumzwa juzi jijini Dar
es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Injinia Joseph Nyamhanga wakati wa mahafali ya 11 ya chuo hicho.
Eng. Nyamhanga alichukua fursa hiyo akimwalisha Waziri wa wizara
hiyo Makame Mbarawa ambaye alikuwa katika majukumu mengine ya
kiserikali.
Katika mahafali hayo, Eng.
Nyamhanga hakusita kuutaka uongozi wa chuo hicho kuhakikisha wanatunza
vema vifaa vya kufundishia ili vidumu kwa kipindi kirefu ili ziendelee
kutoa huduma ya mafunzo kwa wanafunzi wengine waliopo na watakaojiunga
na chuo hicho kwa fani mbalimbali za ubaharia.
Aliongeza kuwa kwa sasa Wizara
hiyo inajipanga kwa ajili ya utanuzi wa majengo ya chuo hicho kwa ajili
ya kutoa fursa kupunguza changamoto ya ufinyu wa madarasa kutokana na
ongezeko la wanafunzi.
Aliongeza kuwa licha ya kuwa katika mchakato huo, eneo la chuo
lililoko Mkuranga nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam tayari wakazi
husika waliokuwa wakimiliki eneo hilo wameshalipwa kwa asilimia 98 hali
inayotoa fursa kwa chuo hiyo kujipanga zaidi kuboresha mahitaji ya chuo
hicho.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho, Meja Jenerali
mstaafu Ligata Sande alisema kuwa chuo kinajipanga kuweka mifumo makini
kwa ajili ya maendeleo yanayohitajika sanjari na kutoa wahitimu wenye
sifa stahiki watakaoweza kupambana na soko la ajira ndani na nje ya
nchi.
Pia msoma risala kwa upande wahitimu Amani Mshana, alisema
wanafunzi wa DMI wanakabiliwa na changamoto ya kutoshirikishwa kwa
katika vikao vya bodi kutokana na kukosekana kwa mwakilishi hali ambayo
inasababisha wanafunzi kushindwa kuwasilisha matatizo yao kwenye bodi ya
usimamizi wa chuo na kushindikana kutotekelezwa kwa mahitaji yao.
Aliongeza kuwa chuo hicho kina upungufu wa walimu ambapo kwa
sasa mwalimu mmoja anafundisha masomo zaidi ya manne na baadhi yao
hawana sifa stahiki hususan katika shahada ya kwanza ya uhandisi wa meli
na unahodha.
Kutokana na changamoto hizo injinia Nyamuhanga aliwahakikishia
wahitimu hao, changamoto hizo kuzifikisha kwa Waziri kwa ajili ya
utatuzi.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269