Msafara wa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira ukiwasili
katika lango Kuu la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam
kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Viongozi Wakuu wa Jeshi hilo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (kushoto) akimsalimia Naibu Inspekta Generali wa Polisi, D/IGP
Abdulrahman Kaniki wakati Katibu Mkuu huyo akiambatana na Naibu wake,
Balozi Simba Yahya (wakwanza kushoto) walipokuwa wanawasili Makao Makuu
ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Katikati ya Katibu Mkuu na D/IGP ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP
Ernest Mangu ambaye alikuwa anawatambulisha viongozi wakuu wa jeshi
hilo.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (meza kuu kushoto)
akiwaongoza viongozi wakuu wa Jeshi hilo kuimba wimbo wa maadili kabla
ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali
Projest Rwegasira (meza kuu katikati) pamoja na Naibu wake, Balozi Simba
Yahya (kulia meza kuu) kuzungumza na viongozi hao wakati walipofanya
ziara ya kikazi ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (wapili kushoto) akitoa
taarifa ya utendaji kazi wa Jeshi lake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza
kuu) wakati Katibu Mkuu huyo ambaye aliambatana na Naibu wake, Balozi
Simba Yahya (wapili kulia meza kuu) katika ziara ya kikazi Makao Makuu
ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Meja Jenerali Rwegasira
aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanaliondoa tatizo la kuwabambikizia
kesi wananchi linalofanywa na baadhi ya askari wasiokuwa na maadili
ndani ya jeshi hilo, kwa kuwa wanalitia doa jeshi hilo ambalo linasifa
nzuri nchini na nje ya nchi. Kulia meza kuu ni Naibu Inspekta Generali
wa Polisi, D/IGP Abdulrahman Kaniki na kushoto ni Kamishina wa fedha na
Lojistiki wa jeshi hilo, Clodwig Mtweve.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (katikati) akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Polisi
wakiongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (wapili
kushoto) wakati Katibu Mkuu na Naibu wake, Balozi Simba Yahya (wapili
kulia) walipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar
es Salaam leo. Katika hotuba yake, Meja Jenerali Rwegasira aliwataka
viongozi hao kuhakikisha wanaliondoa tatizo la kuwabambikizia kesi
wananchi linalofanywa na baadhi ya askari wasiokuwa na maadili ndani ya
jeshi hilo, kwa kuwa wanalitia doa jeshi hilo ambalo linasifa nzuri
nchini na nje ya nchi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(kulia) akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani)
wakiongozwa na Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu (kushoto) wakati
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Rwegasira (katikati) pamoja na
Naibu huyo walipofanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Makao Makuu ya
Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Balozi Simba
aliwataka viongozi hao wa jeshi kupambana na wezi wa mitandao ili
kuusambaratisha mtandao huo nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (kulia) akimuaga Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest
Mangu pamoja na viongozi wengine wa jeshi hilo mara baada ya Katibu Mkuu
huyo ambaye aliambatana na na Naibu wake, Balozi Simba Yahya (katikati)
kumaliza ziara ya kikazi iliyofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya
Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
……………………………………………………………………………………….
Na Felix Mwagara
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali
Projest Rwegasira amewataka viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi nchini
kuhakikisha wanawachukulia hatua kali askari polisi wenye tabia ya
kuwabambikizia kesi wananchi.
Meja Jenerali Rwegasira alisema Jeshi hilo lina sifa nzuri nje
ya nchi pamoja na hapa nchini lakini kuna baadhi ya askari
wasiowaadilifu wanawaonea wananchi mitaani wasiokuwa na hatia kwa
kuwabambikizia kesi ambapo wanalitia doa jeshi hilo.
“Jeshi letu lina sifa nzuri, niliwahi kwenda nchini Kenya
nikaambiwa Jeshi la Polisi Tanzania lina maadili kwani hata likimkamata
mhalifu linafuata sheria na utaratibu na sio kutumia nguvu kubwa kama
yalivyo majeshi mengine,” alisema Rwegazira.
Rwegasira aliongeza kuwa, amefurahishwa sana na utendaji kazi wa
jeshi hilo na kutaka kuongeza umakini zaidi ili kuliletea sifa zaidi
jsehi hilo na yeye yupo karibu nao katika kuliendeleza jeshi hilo ili
liweze kufanya kazi kwa weledi.
Alisema kuwa ni askari wachache mno wenye tabia hiyo ya
kuwabambikizia kesi wananchi na kutofuata sheria za jeshi, hivyo kazi ya
kupambana na askari hao inawezekana endapo viongozi wa jeshi wakiamua
kulifanyia kazi.
“Utendaji kazi wenu ni mzuri, nawapongeza sana hasa
mlivyosimamia uchaguzi mkuu vizuri kwani wananchi wengi walikuwa na
wasiwasi kuhusu usalama wao katika kipindi cha uchaguzi, lakini
mlisimama imara kuhakikisha uchaguzi unamalizika salama,” alisema
Rwegasira.
Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya
naye alitoa pongezi kwa jeshi hilo na kuwataka kuyapeleka mahitaji yao
katika ofisi ya Katibu Mkuu pamoja na yeye ili waweze kuyafanyia kazi na
hatimaye kuliboresha jeshi hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi hilo nchini, IGP Ernest Mangu
aliwapongeza Viongozi hao wa Wizara kwa kuwatembelea katika ofisi za
Makao Makuu ya Jeshi kwani wamefariji na kuwahakikishia viongozi hao
kuwa wamejipanga vizuri katika kulinda usalama wa raia na mali zao na
watayafanyia kazi maagizo waliyopewa.
Katibu Mkuu pamoja na Naibu wake wanamekamilisha ziara yao ya
kuzitembelea Idara za Wizara hiyo ambazo ni Jeshi la Polisi, Jeshi la
Magereza, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ambapo lengo la ziara hizo ni
kujitambulisha kwa viongozi hao pamoja na kujifunza kazi mbalimbali
zinazofanywa na idara hizo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269