Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Shinyanga.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga
Mpina, ameupongeza Uongozi na wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi kwa
kuzingatia sheria za mazingira Mgodini hapo.
Pongezi
hizo alizitoa wakati alipofanya ziara ya kushitukiza katika Mgodi huo
kwa lengo la kujionea namna mwekezaji huyo anavyozingatia maelekezo ya
wataalamu wa wizara yake juu ya utunzaji wa mazingira.
Akiwa
katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alitembelea bwawa maalumu kwa ajili
ya kuhifadhia maji yalitumika kuchenjulia dhahabu na kujionea namna
ambavyo mgodi huo unavyochukua tahadhari ya hali ya juu katika
kuhakikisha maji yanayohifadhiwa ndani ya bwawa hilo hayawezi kuwa na
madhara kwa Jamii, pia naibu Waziri huyo alitembelea kituo cha udhibiti
taka, Uwanda wa kuvuna maji ya mvua mgodini hapo pamoja na karakana ya
mgodi huo.
“Bwawa hili kama unavyoliona usanifu wake, umezingatia tahadhari
zote kuhakikisha hakuna maji yoyote yanatoka nje na hasa ukizingatia
maji yanayopatikana hapa ni yenye mchanganyiko wa madawa yanayotumika
kuchenjua dhahabu” Alisema Meneja wa Kituo cha Uchenjuaji dhahabu bwana
Festo Shayo, wakati alipokuwa akitoa maelezo juu bwawa hilo.
Kwa
upande wake naibu Waziri Mpina amesema licha ya kufanya ziara katika
Migodi mingi bwawa la kuhifadhia maji yanayotoka katika kinu cha
kuchenjulia dhahabu la Buzwagi ni la kiwango cha juu na ameitaka Migodi
mingine pia kutembelea kwa lengo la kujifunza usanifu wake.
“Ni
seme tumepita maeneo mengi ila hapa mmejitahidi kuhakikisha wananchi
wanaowazunguka wako salama, nafikiri kuna haja ya migodi mingine kuja
kujifunza hapa, karakana yenu pia ni nzuri na inazingatia utunzaji wa
mazingira. Alisema mh Mpina.
Aidha
akiwa katika kituo maalumu cha udhibiti taka Mgodini hapo Naibu Waziri
huyo ameutaka uongozi kujenga paa kwenye eneo la udhibiti wa taka za
vyuma ili kuzuia maji ya mvua kugusa taka hizo.
“Mmejitahidi
kuhakikisha taka zinawekwa katika utaratibu mzuri, ila kukosekana kwa
paa hapa ni tatizo, hivyo nawaagiza ndani ya siku therathini eneo hili
liwe na paa” alisema Naibu Waziri Mpina.
Awali
akiukaribisha ugeni wa naibu Waziri huyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa
Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo alimueleza naibu Waziri huyo kuwa sekta ya
madini kwa sasa duniani imekumbwa na changamoto ya kuporomoka kwa bei
ya dhahabu, hali ambayo imepelekea wawekezaji wengi kujikuta
wakijiendesha kwa hasara.
“Mheshimiwa
naibu Waziri, Mgodi wa Buzwagi toka uanze shughuli zake umekuwa
ukishirikiana na Jamii katika kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo
na tunaendelea kufanya hivyo, Hata hivyo changamoto ni kubwa kwani kila
siku bei ya dhahabu inashuka na hii inatufanya tushindwe kujiendesha kwa
faida”alisema Mwaipopo.
“Tumeanza
mchakato wa maandalizi ya kusitisha shughuli za uchimbali maana gharama
zinazidi kuwa kubwa hata hivyo kama bei ya soko itabadilika tutafikiria
vinginevyo” aliongeza Mwaipopo.
Akizungumzia
hatua ya mgodi huo kutaka kusitisha shughuli za uchimbaji naibu Waziri
Waziri ofisi ya makamu wa rais anaeshughulikia mazingira na muungano
Luaga Mpina, amewaomba wawekezaji hao kuangalia namna ingine
itakayowawezesha kuchimba kwa gharama ndogo inayoendana na bei ya
dhahabu.
“kwa
kweli serikali inawahitaji sana wawekezaji na tunaposikia mnaondoka
kwetu sisi ni hasara kwa sababu kodi mbalimbali ambazo mmekuwa mkilipa
kwa halmashauri ya mji wa Kahama hazitakuwepo tena na hii itafanya
miradi mingi ya Maendeleo isitekelezeke baada ya ninyi kuondoka,
tunawaombea bei ya dhahabu ipande ili muendelee kuwepo” Alisema Mpina.
Ziara
hiyo ya kushitukiza ili lenga kujionea namna ambavyo mgodi wa Buzwagi
unazingatia maelekezo mbalimbali ya wataalamu wa wizara yake.
|
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269