Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Mhe. Balozi Simba Yahya
akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza mara baada ya kuwasili
gerezani hapo kwa ziara ya kikazi Januari 29, 2016 kujionea ujenzi wa
mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete lililopo Wilaya ya
Kilombero, Mkoani Morogoro(anayefuatia) ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba
Yahya(wa pili kulia) akiwa ameongozana na Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kushoto) kuelekea
katika Ukumbi wa Gereza hilo kwa ajili ya kupata taarifa kamili ya
utekelezaji wa mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete kutoka kwa
Wakandarasi wa mradi na Mshauri Mwelekezi mradi(kulia) ni Katibu Tawala
wa Wilaya ya Kilombero, Bw. Yahya Sinaniya.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya
akiangalia sehemu ya banio la kutunzia maji ya mradi wa Gereza la Kilimo
Idete akiwa pamoja na msafara wa Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi(wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Kitengo cha
Manunuzi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Manyama Mapesi(wa pili
kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa.
Muonekano
wa mfereji wa maji yatakayokuwa yakitumika katika mradi wa umwagiliaji
wa Gereza la Kilimo Idete, Mkoani Morogoro kama inavyoonekana katika
picha.
Mshauri
wa Mradi, Mhandisi Nzobonaliba Imani akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya(katikati)
alipotembelea mradi wa umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete lililopo
Mkoani Morogoro(kulia) ni Mkuu wa Gereza hilo, Mrakibu Mwandamizi wa
Magereza, Nsajigwa Mwakenja wakiaangalia ujenzi wa mradi wa umwagiliaji
wa Gereza hilo
Wakandarasi
wa Kampuni ya ujenzi wa mradi wa umwagiliaji wa Gereza Kilimo Idete,
lililopo Mkoani Morogoro wakiendelea na ujenzi wa mifereji ya maji kama
inavyoonekana katika picha.
Wajumbe
wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakipata maelezo
ya Kitaalam kutoka kwa Mshauri Mwelekezi walipotembelea mradi huo
kujionea hatua mbalimbali za ujenzi. Wengine ni Wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kilombero.
……………………………………………………………………….
Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Morogoro
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba
Yahya amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya “Tanzania Building Works ya
Jijini, Dar es Salaam” inayojenga mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo
Idete kuukamilisha mradi huo katika muda walioongezewa ili kuwezesha
kuanza kwa shughuli za uzalishaji gerezani hapo.
Akizungumza na Wakandarasi wa
Kampuni hiyo alipofanya ziara ya kikazi Gereza Idete, Balozi Yahya
amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo ni mkombozi kwa Jeshi la Magereza
kwani utawezesha uzalijashi wa chakula cha kutosha cha wafungwa waliopo
magerezani pamoja na kuzalisha ziada itakayouzwa kwa Wananchi ili
kuongeza Mapato Serikalini.
“Ni matarajio yangu kuwa
Mkandarasi wa Mradi huu kwa kushirikiana na Mshauri Mwelekezi na Wadau
wa Jeshi la Magereza atakamilisha mradi huu kwa wakati kama
alivyotuahidi hivyo kuanza mara moja shughuli za uzalishaji”.
Alisisitiza Balozi Yahya.
Naye Msimamizi wa mradi huo
Mhandisi Lodia Mallion alisema kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia
60 ambapo tayari uchimbaji na ujenzi wa mifereji itakayokuwa ikipitisha
maji kwenda mashambani imekwisha kukamilika.
“Mito inayotumika kama vyanzo vya
maji ni mto Kilombero pamoja na mto Kiwiliwili ambapo banio linalotunza
maji kwa shughuli za umwagiliaji tayari limekamilika”. Alisikika
Mhandisi Mallion.
Awali Mkuu wa Gereza Idete,
Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja akiwasilisha taarifa
kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi
Yahya amesema kuwa kazi ya kuandaa mradi huu ilianza rasmi mwaka 2013
ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika Mwaka huu 2016 ambapo gharama za
mradi huo zinakadiriwa kufikia kiasi cha Tsh. 2.5 Bilioni.
Aidha amesema kuwa chakula
kitakachopatikana katika mradi huo wa Gereza Idete kitatumika kulisha
wafungwa waliopo magerezani na ziada itakayopatikana itauzwa kwa
Wananchi hivyo kuongeza pato la Taifa.
Gereza la Kilimo Idete lipo
Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro linajishughulisha na Kilimo cha
mpunga wa chakula na pia mpunga kwa ajili ya mbegu bora za Kilimo hapa
nchimi. Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1983 kwa ajili ya Kilimo
cha mazao mbalimbali hususani Kilimo cha mpunga.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269