Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizungumza na wanahabari ofisini
kwake kuhusu ugeni wa Waziri mkuu ,Majaliwa Kassim Majaliwa mkoani
Kilimanjaro.
Baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi Makala ali-pozung4umza nao ofisini kwake.
……………………………………………………..
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
WAZIRI mkuu, Majaliwa Kassimu
Majaliwa, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ibada maalum ya
kumuingiza kazini askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kiluteri
Tanzania(KKKT),Askofu Dk Frederick Shoo katika kanisa kuu la Moshi
mjini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro, Amos Makalla,amesema waziri mkuu anatarajiwa kuwasili
mkoani Kilimanjaro kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Kilimanjaro(KIA) ambapo atapokea taarifa ya mkoa kabla ya kufanya
shughuli za kanisa.
Alisema waziri mkuu hataongozana na waziri yeyote wa serikali ya
awamu ya tano bali wasaidizi wake na baada ya ziara hiyo maalum
atarejea Dodoma kuendelea na shughuli za serikali.
Ibada hiyo maalumu itajumuisha viongozi mbalimbali wa serikali
ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro sanjari na viongozi wa madhehebu
tofauti ya dini,wadau wa maendeleo,waumini na wananchi kwa ujumla.
Kutokana na ujio huo wa waziri mkuu, mkuu wa mkoa,aliwataka
wananchi hususani katika wilaya za Hai na Moshi kujitokeza kwa wingi
kumpokea kiongozi huyo ambaye pia atapokea changamoto mbalimbali
zinazoukabili mkoa
Kadhalika waziri mkuu anatarajiwa kutoa maelekezo ya serikali
kulingana na changamoto zitakazojitokeza wakati anapewa taarifa ya mkoa.
Dk Shoo ambaye pia ni askofu wa dayosisi ya Kaskazini
amechaguliwa kuongoza kanisa hilo kwa miaka minne na anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na mtangulizi wake askofu Dk Alex Malasusa ambaye
amemaliza muda wake wa uongozi.
Askofu Dk Shoo alichaguliwa mapema mwezi Agosti mwaka jana
katika mkutano mkuu wa 19 wa kanisa hilo uliofanyika chuo kikuu cha
Tumaini jijini Arusha baada ya kuwashinda wenzake wawili.
Uchaguzi wa nafasi hiyo uliwashindanisha askofu Dk Stephen Munga
wa dayosisi Kaskazini Mashariki na Askofu Charles Mjema wa dayosisi ya
Pare.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269