Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro Eng. Dorothy Ntenga
akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa namna maji yanavyopiga kingo za daraja la Dumila wakati Waziri
huyo akikagua ujenzi wa kingo mpya zinazojengwa kudhibiti mafuriko hayo.
Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng. Leornad Chimagu
(kulia),akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa kuhusu athari za mafuriko katika kingo za
barabara ya Gairo-Dodoma eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.
Muonekano
wa Daraja la Dumila mkoani Morogoro lilivyo sasa kufuatia mvua
zinazonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kusababisha mafuriko
yanayoelekea katika Mto Mkondoa.
Mafundi
wakiendelea na ujenzi wa kingo za barabara zilizo athiriwa na mvua
zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kusababisha
uharibifu wa barabara katika eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia),
akitoa maelekezo kwa Meneja wa TANROADS mkoa wa Dodoma Eng. Leornad
Chimagu kuhusu ujenzi wa kingo za barabara hiyo kabla hazija athiri
huduma za usafirishaji.
Gari likipita sehemu iliyoathirika zaidi katika eneo la Kibaigwa barabara kuu ya Gairo-Dodoma.
Magari
yaliyoegeshwa katika kingo za barabara yanavyochangia uharibifu wa
barabara na kusababisha ajali, hili ni eneo la Kibaigwa mkoani Dododma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
………………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemwagiza Meneja wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu
kuhakikisha ukarabati wa barabara katika eneo la Kibaigwa unaanza
jumapili.
Profesa Mbarawa ameyasema hayo
alipokuwa akikagua athari za uharibifu wa barabara zilizosababishwa na
mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Iringa – Dodoma na
kusababisha mafuriko yanayoharibu kingo za barabara.
“Hakikisheni Jumapili kazi ya
ujenzi hapa inaanza na ikamilike kwa muda mfupi ili kutoathiri huduma ya
usafiri katika barabara hiyo kutokana na umuhimu wake”, alisema Prof.
Mbarawa.
Waziri Mbarawa amewataka TANROADS
washirikiane na Kikosi cha Usalama Barabarani kudhibiti magari
yanayoegeshwa katika maeneo yasiyo rasmi na hivyo kusababisha ajali na
uharibifu wa barabara hususani katika maeneo ya Dumila mkoani Morogoro
na Kibaigwa mkoani Dodoma.
Mapema Waziri Mbarawa alikagua
ujenzi wa kingo za barabara unaoendelea katika eneo la Dumila mkoani
Morogoro ambapo amemuagiza Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro Eng.
Dorothy Ntenga kuhakikisha ujenzi huo wa kudhibiti barabara na daraja la
Dumila unakamilika kabla ya Februari 15 ili kukabiliana na mafuriko
wakati wa mvua za masika zinazokaribia kuanza.
“Chimbeni mchanga kwenye mto ili
kuwezesha maji kupita kwa urahisi na kuondoa tishio la mafuriko yanayo
athiri daraja hilo wakati wa mvua za masika”, alisisitiza Waziri
Mbarawa.
Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa
Morogoro, Eng. Dorothy Ntenga amesema ili kudhibiti mafuriko katika eneo
la Dumila juhudi zinaendelea kupunguza mchanga na hivyo kuwezesha
kupita maji kwa urahisi.
Profesa Mbarawa alikuwa katika
ziara ya kukagua athari za mafuriko katika barabara ya Morogoro-Dodoma
ambapo maeneo ya Dumila na Kibaigwa yameathirika zaidi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269