Baadhi ya wanamauzo wa kanda ya pwani ya Tigo wakiwa katika picha ya pamoja siku ya mahafali yao ya kuhitimu mafunzo maalum ya ujasiriamali yaliyotolewa na Tigo |
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
jitihada
za kuwawezesha wafanyakazi wake wa kujitegemea kumudu changamoto mbalimbali za
kikazi na kimaisha, Tigo imewapa wafanyakazi hao wapatao 4,767 mafunzo maalum
ya ujasiriamali kupitia mpango wake wa mafunzo kazini.
Mpango wa Tigo
wa mafunzo kazini kwa wanamauzo wakujitegemea uitwayo Tigo Sales School (TSS) ulianzishwa mwaka 2012 ambapo kwa mujibu wa
Meneja wa TSS Justine Kwizera, kampuni inatarajia kutoa mafunzo hayo kwa
wanamauzo wake wote wapatao 10,000 katika kipindi cha miaka
mitatu ijayo.
Alisema kila
mwaka Tigo huwekeza kiasi cha 600m/- katika mpango huu ikiwa ni sehemu ya
mkakati wa kampuni hiyo wa kuimarisha utoaji huduma kwa wateja wake. Tigo ina
zaidi wateja milioni kumi.
“Mpango wa TSS
unalenga katika kuwajengea uwezo wa kiutendaji kazini wanamauzo wa kujitegemea
wa Tigo pamoja kuwapa mbinu za kujikimu katika kukabiliana na changamoto
mbalimbali maishani,”amesema Kwizera katika mahojiano maalum.
Mafunzo
yanayotolewa na TSS ni pamoja na stadi za mauzo, ujasiriamali, usimamizi wa
fedha na huduma kwa wateja, alisema Kwizera na kuongeza kwamba mafunzo hudumu
kwa muda wa siku nane darasani na kufuatiwa na mafunzo kwa vitendo
kwa miezi mitatu.
“Mafanikio
ambayo tumeyashuhudia kutokana na mafunzo haya ni ongezeko kubwa la mauzo na
kuimarika kwa huduma kwa wateja sambamba na mabadiliko chanya katika hali ya
maisha ya wanamauzo wetu,” alisema meneja huyo wa TSS.
Aidha alisema
Tigo inaendeleza kutoa mafunzo kwa wanamauzo katika kila duka na ofisi zake 24 za
mauzo nchi nzima ili kuendeleza watendaji
wakezaidi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269