Mjane Tabu Salum Tambwe |
Dotto Mwaibale
MTU
mmoja ambaye ametajwa kuwa ni raia wa Kenya anadaiwa kuiteka Manispaa
ya Ilala kwa kushiriana na watendaji wasio waaminifu wa manispaa hiyo
kudhulumu viwanja vya watu eneo la Pugu Mwakanga.
Raia
huyo wa Kenya ametajwa kuwa ni Phinians Otieno ambaye amefungua ofisi
yake eneo la Pugu Kinyamwezi Chanika ili kuwa jirani na viwanja ambavyo
inadaiwa anaviuza kiujanjajanja kwa kushirikiana na watendaji wa
manispaa hiyo wasio waaminifu akiwemo ofisa ardhi mwandamizi mmoja na
ofisa mwingine wa manispaa hiyo ambao majina yao yanahifadhi.
Imeelezwa
kuwa katika manispaa hiyo mkenya huyo ana ndugu zake watano ambao
wameajiriwa hapo akiwepo shemeji yake ambao wanampa siri ya viwanja
vilipo na kukamilisha udhulumaji wa viwanja vya wananchi hasa katika
maeneo ambayo hayajapimwa na amekuwa akitamba kuwa hakuna mtu wa
kumbabaisha kwani hata waziri Lukuvi anafahamiana naye.
Imedaiwa
kuwa raia huyo wa kenya aliingizwa katika mchongo huo wa viwanja na
kigogo mmoja wa manispaa hiyo ambaye alitimuliwa kutokana na kujihusisha
na vitendo vya rushwa ambaye alimpa tenda ya kuwapimia viwanja wananchi
waliohamishwa Kipawa kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege katika eneo hilo
la Pugu Mwakanga na baada ya kupima viwanja hivyo ameingia eneo la
wakazi wa Mwakanga akidai ni lake.
Katika
tukio la aina yake ni jaribio la mkenya huyo la kutaka kumpora viwanja
mjane mmoja wa eneo hilo Tabu Salum Tambwe (pichani) akidai ni vyake kwa
kushirikiana na baadhi ya watendaji wa manispaa hiyo.
Viwanja
vya mjane huyo ambavyo anataka kudhulumiwa na mkenya huyo ni 869-876
vilivyopo Kitalu 'N' Pugu Mwakanga ambavyo mjane huyo amekuwa akivilipia
kodi tangu avinunue lakini kutokana na mchezo mchafu unaofanywa kwa
ajili ya kutaka kumdhulumu amekuwa akipigwa chenga ya kumilikishwa licha
ya kutoa zaidi ya sh.milioni 21.
Akizungumza
na gazeti hili Tambwe alisema amepoteza fedha nyingi kwa ajili ya
kupata umilikishwaji wa viwanja hivyo ambavyo anataka kudhurumiwa.
Tambwe
alisema kuwa tangu avinunue viwanja hivyo mwaka 2007 amekuwa akivilipia
kodi na mara ya mwisho kuvilipia ilikuwa mwaka juzi ambapo alilipa
sh.640,000 na kukabidhiwa stakabadhi namba 356568, 356569, 356570,
356565, 356567, 356565, 356563.
Mjane
huyo alisema changamoto kuwa iliyopo ni kuhusu umilikishwaji wa viwanja
hivyo ambapo aliambiwa ni lazima alipie kabla ya kupewa ofa ambapo
katika kiwanja namba 872 alilipa sh.224,402.80, 876 alilipa
sh.281,118.40, 870 alilipa sh. 247,964.80, 874 alilipa sh. 244, 567.20,
875 alilipa sh. 303,668.40, 873 alilipa sh.270,350.40 na kiwanja namba
871 alilipa sh.270,131 jumla ikiwa ni sh.milioni 21.2 fedha alizolipa
kwa mkabidhi keshia mmoja ambaye yupo dirisha la malipo aliyemtaja kwa
jina moja la Fatuma lakini hadi leo hii bado hajamilikishwa.
Hata
hivyo baadhi ya maofisa wa manispaa hiyo wameoneshwa kukerwa na vitendo
vinavyofanywa na mkenya huyo kwa kushiriana na wenzao na wamesema kuwa
wapo tayari kutoa ushirikiano kwa Waziri Lukuvi ili kumsaidia mjane huyo
apate haki yake kwani katika manispaa hiyo wao wanaonekana kama ni
takataka na mkenya huyo anaonekana ni mungu mtu.
"Tunawaombeni
wanahabari mutusaidie katika jambo ili kwani watu wengi wanaendelea
kuumizwa na watendaji wenzetu wasio waaminifu wakishirikiana na mkenya
huyo ambaye si raia hapa nchini lakini amekuwa milionea kwa kuuza ardhi
kiujanjaujanja sisi tupo tayari kusema ukweli" alisema ofisa mmoja wa
manispaa hiyo kwa uchungu.
Imeelezwa
kuwa mkenya huyo kwa wakazi wote aliyewauzia viwanja katika eneo hilo
amekuwa akiwatoza kodi ambayo ilipaswa kulipwa serikalini lakini
uichukua na kuitia mfukoni mwake.
Mjane
huyo anamuomba Waziri Lukuvi kumsaidia ili apate haki yake ambayo ipo
hatarini kupotea kupitia watumishi wa waliochini ya wizara yake
wanaoshirikiana na raia huyo wa Kenya.
Akitoa
ufafanuzi wa madai hayo mkenya huyo alidai kuwa mama huyo alitapeliwa
kwa kuuziwa viwanja hivyo ambavyo si vyake na mtu mmoja aliyemtaja kwa
jina la Dullah na kwamba yeye alikuwa akimsaidia ili kupata haki yake.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269