·
NA K-VIS MEDIA Na Mashirika ya Habari
·
·
JAJI wa Mahakama Kuu nchini Kenya
Philip Tunoi(Pichani), mwenye umri wa miaka 72 anatuhumiwa kula “kula_ mlungula
kiasi cha shilingi za Kenya Milioni 2.
·
·
Jaji huyo ambaye anatarajiwa kufikishwa
mbele ya Tume ya Huduma za Mahakama (Judiciary Service Commission-JSC),
Jumatano Januari 27, 2016, amewatuhumu baadhi ya majaji wenzake kuwa ndio
walioanzisha “figisufigisu” ili yeye aondolewe na wachukue nafasi yake. Gazeti
la Standard la Kenya limeripoti leo
Jaji huyo
ameendelea kujitetea kuwa kundi hilo la majaji na baadhi ya mawakili, wamefikia
hadi kuomba afe kwa vile tu alikataa kustaafu wakati akiwa na umri wa miaka 70.
Tuhuma
zenyewe ni kwamba, jaji huyo mashuhuri nchini Kenya, alipokea rushwa ya shilini
milioni 200 kutoka kwa Gavana wa Nairobi Evans Kidero ili kupindisha matokeo ya
pingamizi mbunge wa Kabete, Ferrdinand Waititu akipinga kuchaguliwa kwa Gavana
huyo na kutuhumu kuwa Gavana huyo alimtumia mu mmoja aitwaye Geofrey Kiplagat.
Kwa mujibu
wa gazeti hilo, limemnukuu Bw. Kiplagat akisema kuwa sekeseke hilo la rushwa
lilianza mwezi Mei, 2014 ambapo aliombwa na mfanyabiashara mmoja kupitia njia
ya simu kama ataweza kumuunganisha na Jaji Tunoi kumsaidia kwenye kesi dhidi ya
Dkt. Kidero.
Kiplagat
ameliambia gazeti hilo kuwa baada ya kukamilisha mipango hiyo na kwenda sawa,Jaji
huyo alikabidhiwa mlungula huo (rushwa), kwenye kituo kimoja cha mafuta jijini Nairobi.
Kufuatia
tuhuma hizo, gazeti hilo limeripoti leo kuwa Jaji Mkuu wa Kenya, Dkt. Willy Mutunga, ametangaza
kikao maalum cha kamati ya huduma za kimahakama
itakaa kushughulikia suala hilo ambalo limeichafua Mahakama Kuu ya
Kenya.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269