Ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Afrika nchini Uganda
umetoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujitokeza kwa wingi na kutimiza haki
yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi wawapendao.
Mkuu wa ujumbe huo wa AU, Sophia Okofor pia amewataka raia wa Uganda
kudumisha amani na kuwa watulivu baada ya uchaguzi. Bi. Okofor kutoka
Ghana aidha amewataka wanasiasa wanaowania nyadhifa mbalimbali kuheshimu
matokeo na kufuata mchakato wa kisheria endapo hawataridhishwa na
matokeo ya uchaguzi.
Uchaguzi wa bunge na rais umeanza asubuhi ya leo nchini Uganda na
tayari Rais Yoweri Museveni amepiga kura yake katika kituo cha Rwakitura
huku wagombea wengine wa nafasi ya urais pia wakipiga kura zao kwenye
vituo walikosajiliwa.
Wapigakura waliojiandikisha ni takriban milioni 15.3 na kuna vituAo
28, 010 kote nchini Uganda. Wagombea urais ni wanane na kwa upande wa
bunge, viti vinavyowaniwa ni 290.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269