Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika kadhia ya Yemen amesema
kuwa, duru ya pili ya mazungumzo kati ya pande zinazohasimiana
imeshindwa kufanyika kutokana na Saudi Arabia kukataa kutoa hakikisho la
kusitisha vita.
Ismail Ould Cheikh Ahmed amesema upande wa Mahuthi unataka duru
ya pili ya mazungumzo ifanyike kwa sharti kwamba vita visimamishwe. Hata
hivyo, mwanadiplomasia huyo wa UN amesema Saudi Arabia inasisitiza
kufanyika duru hiyo ya pili bila kuweko sharti la usitishwaji vita.
Mara ya kwanza kwa harakati ya wananchi ya Ansarullah ya Yemen
kukutana ana kwa ana na serikali iliyojiuzulu na kukimbia nchi ilikuwa
mwezi Disemba mwaka jana huko nchini Uswisi ambapo pande mbili hizo
zilishindwa kufikia natija yoyote. Hadi sasa mjumbe wa UN hajasema ni
lini duru ya pili ya mazungumzo itafanyika.
Huku hayo yakijiri, Saudi Arabia imeendelea kushambulia makazi ya
raia na vituo vya afya kwenye hujuma yake ya angani dhidi ya watu wasio
na hatia wa Yemen.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269