Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia
aliyevaa kiraia) akiingia ndani ya Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga mjini
Moshi. Rwegasira amefanya ziara kwa kukitembelea kiwanda hicho kwa lengo la
kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Magereza. (Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
akiangalia buti la Jeshi lililotengenezwa na Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga,
mjini Moshi. Kiwanda hicho kinatengenezwa viatu vya aina mbalimbali. Kushoto ni
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Venance Kayombo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
(kushoto) akimsalimia Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo wakati Kiongozi huyo wa Wizara
alipowasili katika ofisi za Magereza Mkoa, mjini Moshi.
Fundi
wa Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga mjini Moshi, Hashim Rashid akimuonyesha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (kushoto) jinsi buti la Jeshi linavyotengenezwa ndani ya kiwanda
hicho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269