Naibu
waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt Abdallah Possi
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(HawapoPichani) kuhusu vyombo vya
habari kutekeleza Sheria ya Watu wenye Ulemavu katika kupata habari.
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Naibu
waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (WatuwenyeUlemavu) Dkt Abdallah Possi
ameviagiza vyombo vya habari nchini kuzingatia Sheria ya Watu wenye ulemavu kwa
kuhabarisha kwa kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu katika kutoa habari,
Akitoa
agizo hilo mbele ya vyombo vya habari leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam
Waziri Possi amesema vyombo vya habari vinatakiwa kuwakumbuka na watu wenye
ulemavu katika utoaji wa taarifa mbalimbali katika Magazeti, Radio
naTelevisheni hasa kwa kuzingatia lugha za alama ambazo zitawawezesha kuelewa
habari husika.
“ Naomba
tubadilike wanahabari kwa kuwajali watu wenye ulemavu kwa kuwahabarisha na wao
pia, nawataka wamiliki wa vyombo vya habari hususan Televisheni kuweka lugha za
alama kwa ajili ya watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kupata habari mbalimbali
zinazojiri katika taifa”
“Vyombo
vya habari vinatakiwa kubadili uono wao juu ya walemavu na sio kwa kuangalia
mambo hasi tu yahusiyo walemavu kwamba wana shinda,hawawezi, wanahitaji msaada
ila pia kwakuangalia mafanikio yao katika kuleta maendeleo ya taifa kiujumla”
Alisema Dkt Possi.
Aidha Dkt
Abdallah Possi amewataka waandishi wa habari hasa wa magazeti kuzingatia lugha
wanazotumia kandika habari za watu wenye ulemavu ili kuondoa fikra na
dhana hasi na unyayapaa juu ya walemavu huku akitolea mfano baadhi ya lugha
zinazotumika na baadhi ya waandishi katika kuandika habari zinazohusu watu
wenye ulemavu kuwa hazistahili.
Ametaja
mfano wa lugha ambazo sio sahihi katika uandishi wa habari za wenye ulemavu
mfano maneno vipofu, viziwi,vilema na maneno mengine bali wanatakiwa kutumia
maneno yenye staa na yasiyoleta picha ya unyanyapaa na udhalilishaji kwa watu
wenye ulemavu ili kuondokana na dhana ya unyanyapaa na udhalilishaji wa watu
wenye ulemavu.
Kupata
habari ni haki ya kila mtu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Sheria No 9 ya Mwaka 2010 inavitaka vyombo vya habari kuhabarisha
watu bila kuwabagua watu wenye ulemavu, tuelewe kwamba pia watu wenye ulemavu
wana haki ya kupata taarifa kama watu wengine.
Serikali yaagiza vyombo vya
habari kuzingatia Sheria ya watu wenyeUlemavu
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269