Marekani na Cuba
zimetiliana tena saini makubaliano ya kurejesha tena safari za ndege za
abiria baina ya nchi hizo mbili kwa mara ya kwanza katika kipindi cha
miaka hamsini iliyopita.
Utiwaji wa saini ya makubaliano hayo
ulikuwa ni baina ya waziri wa usafiri wa Marekani , Anthony Foxx na
mwenziwe kutoka Cuba Adel Izquierdo Rodriguez, mjini Havana makubaliano
hayo yatashuhudia safari lufufu za kila uchao baina ya mataifa hayo
yaliyokuwa mahasimu hapo awali.
Matarajio ya kuanza kwa safari
hizo ni baada ya mwezi mmoja,ingawa mpaka sasa kisheria ni Marufuku kwa
raia wa Marekani kuitembelea Cuba kama mtalii.
Ki diplomasia
uhusiano wa nchi mbili hizo ilianza kurejea zaidi ya takribani mwaka
mmoja uliopita .Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Havana ameelezea juu ya
makubaliano hayo ya hivi karibuni kwamba yamekuja baada ya ikulu ya
Marekani kutafakari uwezekano wa safari za kiserikari za rais wa Cuba
nchini Marekani. |
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269