Rais Barack Obama amesema anaamini mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump hatakuwa rais wa Marekani.
Amesema kazi hiyo ni “kazi kubwa”.
"Ninaendelea kuamini kwamba Bw Trump hatakuwa rais. Na sababu ni kwamba nina imani sana na Wamarekani,” amesema Bw Obama.
Bw
Trump, mfanyabiashara tajiri sana kutoka New York, anaongoza kwenye
kura za maoni katika kinyang’anyiro cha kuteua mgombea wa chama cha
Republican.
- Trump alidhani mji wa Paris uko Ujerumani?
- Wabunge Uingereza wamjadili Trump
- Wagombea wamkejeli Trump kwenye mdahalo
Tayari ameshinda uchaguzi wa mchujo jimbo moja, na anaongoza
kwenye kura za maoni jimbo la South Carolina, ambako wafuasi wa
Republicans watashiriki uchaguzi wa mchujo Jumamosi.
Akiongea
wakati wa mkutano mkuu wa kiuchumi wa nchi za kusini mashariki mwa Asia
unaofanyika katika jimbo la California, rais aliulizwa na mwanahabari
kumhusu Trump.
Watu hawatampigia kura, alisema Bw Obama, kwa sababu “wanajua kuwa rais ni kazi kubwa”.
"(Kazi
hii ) Si kama kuzungumza katika kipindi cha runinga, si matangazo au
mauzo ya bidhaa, ni kazi ngumu. Si kazi ya kushawishi watu na kufanya
utakalo ndipo utokee kwenye vichwa vya habari siku fulani.”
Bw Trump amemjibu na kusema ni kama kusifiwa iwapo utakosolewa na rais ambaye ameharibu sana nchi.
Mwanasiasa
huyo anamchukia sana Obama na miaka ya nyuma alizoea kumtaka atoe
stakabadhi za kuthibitisha kwamba alizaliwa Marekani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269