Jeshi la Nigeria limesema kuwa
limeharibu kambi za wapiganaji wa Boko Haram katika vijiji vya Doro na
Kuda kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno.
Wapiganaji wanne wa
kundi hilo waliuawa huku wengine wawili wakikamatwa wakati wa oparesheni
katika misitu ya eneo la Alagarno na Sambisa,kulingana na msemaji wa
jeshi kanali sani Usman.
Wanajeshi watatu na raia wanne walijeruhiwa katika mapigano hayo, alisema.
Pikipiki,farasi na Punda walipatikana katika kambi hiyo.
Kundi la Boko haram limepoteza eneo kubwa lililokuwa likidhibiti, lakini bado linatekeleza milipuko mibaya ya kujitolea muhanga.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269