Kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabaab, lilidai kuhusika na
mlipuko huo, lakini halijatoa majina ya waliohusika moja kwa moja.
Hamna aliyeuawa wakati wa mlipuko huo, ambao ulitokea dakika kumi na tano baada ya ndege hiyo kupaa.
Ndege hiyo ililazimika kurejea na kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Mogadishu nchini Somalia.
Mwalimu mmoja wa shule ya Madrasa,
ametambuliwa kuwa mshukiwa aliyetekeleza shambulio la bomu ambalo
lilisababisha shimo kubwa katika tanki ya mafuta ya ndege moja ya abiria
nchini Somalia, iliyokuwa ikielekea nchini Djibouti, tarehe mbili
Februari mwaka huu.
Abdullahi Abdisalam Borleh, alirushwa na
mlipuko uliotokea katika ndege hiyo aina ya Airbus 321, wakati bomu hilo
lilipolipuka muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka uwanja wa
ndege wa Mogadishu.
Maafisa wa idara ya ujasusi wanaamini kuwa
Borley, ambaye anatoka eneo lililojitenga na Somalia la Somaliland,
alibeba bomu hiyo kimakusudi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269