K-VIS
MEDIA Na Mashirika ya Habari
KIONGOZI
wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, amemvaa mgombea urais wa Marekani
Donald Trump, na kumwita sio Mkristo.
Papap
Francis ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ndege akirejea Vatican akitoka nchini
Mexico baada ya kuongoza ibada kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.
Trump
alinukuliwa kuwa akiwa Rais wa Marekani atajenga ukuta kwenye mpaka wan chi yake
na Mexico ili kuzuia wahalifu kuingia Marekani hususan wauza “unga”.
Pia
Papa Francis hakufurahishwa na kauli za mgombea huyo tajiri zinazoashiria
ubaguzi ambapo Trump amewahi kunukluliwa kisema, endapo atachaguliwa kuwa rais
wa Marekani, Waislamu hawataruhusiwa kuinia nchini humo.
Papa
alisema “Yeyote anayefikiria kujenga ukuta baina ya Mexico na Marekani huyo sio
Mkristo.” Papa alisema.
Akijibu
matamshi hayo ya Papa, Trump ambaye alikjuwa akifanya kampeni zake huko South
Carolina, aliiita kauli ya Papap kuwa si ya haki na kumwita Papa kuwa ni “mshenga)
wa serikali ya Mexico”
“Sibabaishwi
na kauli za Papa, ni lazima tuzuie wahamiaji haramu.” Alisema Trump akimjibu
Papa. na kuongeza kuwa Papa atatambua Ukristo wa Trump, pale Vatican
itakaposhambuliwa na Wanamgambo wa Kiislamu, ISIS
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269