Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa jana liliitisha kikao kujadili hali ya mambo nchini Burundi.
Kikao hicho kilichofanyika mjini Geneva Uswisi kilijadili ripoti
ya wataalamu watatu wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa
kuhusiana na hali ya haki za binadamu nchini Burundi. Asasi zisizo za
kiserikali pamoja na nchi wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la
Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Burundi ianzishe mwenendo wa
mazungumzo na wapinzani kwa shabaha ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa
kisiasa wa nchi hiyo.
Kikao hicho kiliashiria pia kuweko kesi za ukiukaji wa haki za
binadamu nchini Burundi sambamba na kutathmini utiwaji mbaroni wapinzani
pamoja mateso wanayokabiliana nayo kutoka kwa vyombo vya serikali.
Machafuko ya ndani nchini Burundi yalianza baada ya Rais Pierre
Nkurunziza wa nchi hiyo kutangaza nia yake ya kuwania tena kiti hicho
kwa mara ya tatu mfululizo. Wapinzani wanasema hatua hiyo ilikiuka
katiba ya nchi na makubaliano ya amani ya Arusha, Tanzania
yaliyohitimisha vita vya ndani katika nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, tangu Aprili mwaka 2015 hadi sasa
wakimbizi laki tano na 946 wa Burundi wamekimbilia katika nchi jirani za
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tanzania, Rwanda, Uganda na Zambia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269