Dkt. Ali Mohammed Shein (pichani),
ametangazwa leo Machi 21, 2016, kuwa ameshinda uchaguzi wa marudio wa
Zanzibar kwa asilimia 91.4, ushindi ambao umeelezwa kuwa ni mkubwa kwa
kiongozi wa Zanzibar usinda katika miaka ya hivi karibuni.
Hata hivyo Dkt. Shein amepata ushindi
huo katika mazingira ambayo, chama kikuu cha upinzani visiwani humo
yaani CUF, kiliususia uchaguzi huo kwa maelezo kuwa uchaguzi wa marudio
si wa haki kwa vile uchaguzi ulikwishafanyika Oktoba 25, 2015 ambapo
chama hicho kilielekea kushinda. Hata hivyo mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar, (ZEC), Jecha Slim Jecha, aliufuta uchaguzi huo kwa
maelezo kuwa ulijawa na ghiliba na haukuwa huru na wa haki.
Dkt. Shein akisalimiana na Hamad Rashid |
Kwa mujibu wa matangazo ya leo ya
matokeo ya uchaguzi huo, Dkt. Shein amekusanya jumla ya kura 299,982
huku anayemfuatia, Hamad Rshid Mohammed, amejipatia kura 9,734 sawa na
asilimia 3.4, huku Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye chama chake
hakikushiriki uchaguzi huo amepata kura 6076 sawa na asilimia 1.9.
Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, chama kinachofuatia kile kilichoshinda, ndicho kitatoa makamu wa kwanza wa rais.
Hamad Rashid Mohammed wa ADC |
Dkt. Ali Mohammed Shein, rais mteule wa
Zanzibar, akionyesha cheti chake cha ushindi mara baada ya kutangazwa
na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Sa,im Jecha kwenye
ukumbi wa Salama wa Hoteli ya Bwawani mjini Unguja Machi 21, 2016.
Mwenyekiti Jecha akitangaza matokeo
Aliyeshika nafasi ya pili kwenye matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar, Hamad Rashid akitoa hotuba yake |
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269