Breaking News

Your Ad Spot

Mar 21, 2016

RAIS MAGUFULI AMUUNGA MKONO MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA KWA AGIZO LA UHAKIKI WA SILAHA, YEYE AWA MTU WA KWANZA KUFANYA HIVYO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiitoa silaha yake aina Bastola kwa ajili ya uhakiki Ikulu jijini Dar es Salaam Machi 21, 2016akitekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, alilolitoa hivi karibuni kuwataka wale wote wanaomiliki silaha kuzihakiki mara moja.Rais amekuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kutekeleza agizo hilo wewe je??. Kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Siro.(Picha na Ikulu).
 Rais akikabidhi silaha yake kwa Kamanda Siro ili ihakikiwe
 Rais akionyesha silaha yake tayari kufanyiwa uhakiki
 Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Neema Laizer (kulia) akiendelea na zoezi la kuhakiki Silaha za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka vizuri silaha yake aina ya Shortgun mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka vizuri silaha yake aina ya Shortgun mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, tayari kwa kuhakikiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kwa makini zoezi la uhakiki wa silaha zake lililokuwa likifanywa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Neema Laizer Ikulu jijini Dar es salaam. Mhe. Rais amekuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza zoezi la kuhakiki silaha zake Ikulu jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Rais amewataka wananchi wote wanaomiliki silaha kujitokeza kuhakiki silaha zao kama alivyoagiza  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages