serikali ya Morocco imetangaza kuwanasa kwa akali watu tisa kwa
kuwa na mahusiano na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh nchini humo.
Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco
imesema kuwa, watuhumiwa hao walitiwa mbaroni na polisi katika mji wa
Marrakesh na miji mingine ya nchi hiyo wakati walipokuwa wakipanga
shambulio la kigaidi. Katika ripoti hiyo, magaidi hao walikuwa
wanakusudia kwenda Libya kwa ajili ya kujifunza mafunzo ya kijeshi.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco imetangaza kuwa, tangu mwaka 2013
hadi hivi sasa, imeshasambaratisha zaidi ya makundi 30 ya kigaidi nchini
humo. Aidha katika kipindi hicho polisi wa nchi hiyo imevunja njama
mbalimbali za kuharibu usalama na amani nchini. Ni vyema kuashiria hapa
kwamba, asilimia kubwa ya wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la
Daesh ni vijana kutoka Tunisi na Morocco.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269