Breaking News

Your Ad Spot

Mar 26, 2016

KUENDELEA MVUTANO WA KISIASA NCHINI LIBYA

Kuendelea mvutano wa kisiasa nchini Libya
Licha ya kuripotiwa habari za kuhamishiwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya katika mji mkuu wa Libya Tripoli katika kipindi cha chini ya wiki moja, Waziri Mkuu wa serikali iliyojitangazia yenyewe mamlaka huko Tripoli, ametangaza hali ya hatari ya usalama katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Khalifa al-Ghwell, Waziri Mkuu wa serikali iliyojitangazia yenyewe mamlaka, jana alitoa taarifa na kutangaza hali ya hatari ya usalama katika nchi hiyo na akavitaka vikosi vya usalama viimarishe doria katika maeneo ya magharibi mwa nchi hiyo. Hivi karibuni, Martin Kobler, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya alisema kuwa, serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya itaundwa katika kipindi cha chini ya wiki moja na kuhamishwa katika mji mkuu Tripoli. Tangazo hilo la Martin Kobler liliungwa mkono na nchi jirani na Libya na hata madola makubwa ulimwenguni. Baada ya tangazo hilo ilitarajiwa kwamba, joto la mgogoro wa kisiasa wa Libya lingepungua na hivyo kushuhudia kufikia tamati kipindi cha utawala wa serikali mbili ambao umekuweko nchini humo tangu Agosti mwaka 2014. Utawala wa serikali mbili nchini Libya mbali na kusababisha kutoundwa serikali ya umoja wa kitaifa umepelekea kushadidisha kiwango cha ukosefu wa usalama na amani katika nchi hiyo.
Magaidi wa Daesh wanadhibuti maeneo mbalimbali ya Libya ukuwemo mji wa Sirte mahala alipozaliwa dikteta wa zamani wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi. Harakati za kundi la Daesh huko Libya zimekuwa na taathira hasi pia kwa usalama wa nchi jirani hususan Tunisia. Fauka ya hayo, mgogoro wa wahajiri haramu na magendo ya binadamu nchini Libya ni mambo ambayo nayo yameshtadi, kiasi kwamba, Jean-Yves Le Drian, Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa amesema kuwa, harakati za kundi la kigaidi la Daesh, wimbi la wahajiri haramu na magendo ya binadamu ni mambo matatu makuu hatari yanayoikabili Libya. Hapana shaka kuwa, mambo hayo yatakuwa na matokeo mabaya pia kwa usalama wa Ulaya.
Filihali, Khalifa al-Ghwell Waziri Mkuu wa serikali ya Libya yenye makao yake Tripoli amepuuzilia mbali vitisho na kuhatarishwa usalama wa raia na wa ardhi ya nchi hjiyo na kutangaza kwamba, hakubaliaini na suala la kuachia madaraka na kukabidhi hatamu za uongozi kwa serikali ya umoja wa kitaifa.
Mwanasasa huyo amekwenda mbali zaidi na kutangaza kuwa, endapo wajumbue wa serikali ya umoja wa kitaifa wataelekea Tripoli kwa ajili ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa basi atawatia mbaroni na kuwatupa korojkoroni.
kwa upande wake Faiz al-Siraj, Mkuu wa Baraza la Uongozi la Libya ametangaza kuwa, serikali ya maafikiano ya kitaifa inatarajiwa kuanza kazi zake huko Tripoli karibuni hivi.
Inaonekana kuwa, katika mazingira ya sasa Libya inakabiliwa na mgogoro wa hisa na nyadhifa katika serikali ijayo ya maafikiano ya kitaifa. Kuna baadhi ya mirengo nchini Libya ambayo inaona kuwa, maslahi yao yatakuwa hatarini endapo kutaundwa serikali ya maafikiano ya kitaifa katika nchi hiyo. Vikosi vya serikali ya Libya yenye makao yake mjini Tripoli ambavyo vikiwa chini ya mwavuli wa muungano wa makundi yenye kubeba silaha unaojulikana kama "Fajr Libi" kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa vimekuwa vikidhibiti akthari ya maeneo ya magharibi mwa nchi hiyo ukiwemo mji mkuu Tripoli vinaona kuwa, vyenyewe vitapata hasara kwa kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa uongozi wa Faiz al-Siraj.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages