Akizungumza Kitwanga amesema kuwa hali ya usalama ni ya uwakika na kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika sherehe za kuapishwa Rais Mteule wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein zinazotarajiwa kufanyika kesho katika uwanja wa Aman mjini Unguja.
Aidha ameongeza kuwa wizara imejipanga kulinda amani na utulivu uliopo sasa Unguja na Pemba na kuwatoa hofu wananchi wa visiwani humo,kwani jeshi la polisi lipo kwa ajili ya kuhakikisha usalama wao na mali zao.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga , akitoka baada kuzungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar jana, kuhusu hali ya usalama ilivyo shwari Pemba na Unguja. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269