Rais Idriss Déby wa Chad ametangazwa kuwa mshindi wa uchagumzi mkuu uliofanyika hivi karibuni nchini Chad.
Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo imemtangaza rais huyo kuwa ndiye
mshindi katika uchaguzi huo na hivyo kuwa rais kwa muhula wa tato
mfululizo nchini Chad. Kwa mujibu wa tume hiyo, Rais Idriss Déby amepata
asilimi 60 ya kura, huku mpinzani wake Saleh Kebzabo akipata asilimia
12 ya kura hizo. Tayari Kebzebo amepinga matokeo hayo akisema kuwa,
kulifanyika uchakachuaji mkubwa wa kura kwa maslahi ya Rais Déby. Aidha
mwanasiasa huyo amesema kuwa mbali na uchakachuaji huo, mamia ya
masanduku ya kura yalipotea, na kusisitiza kuwa, raia wa Chad hawawezi
kukubaliana na matokeo hayo. Wiki iliyopita waangalizi wa Umoja wa
Afrika kwenye uchaguzi huo walinukuliwa wakisema kuwa, uchaguzi nchini
Chad ulifanyika katika anga huru na salama. Itafahamika kuwa, Rais Déby
amekuwa madarakani tangu mwaka 1990, baada ya kumuondoa madarakani
aliyekuwa rais wa nchi hiyo, dikteta Hissène Habré. Uchaguzi Mkuu nchini
Chad ulifanyika tarehe 10 ya mwezi huu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269