Breaking News

Your Ad Spot

Apr 15, 2016

RAIS SALVA KIIR WA SUDAN KUSINI AWASILI NCHINI KUSAINI HATI ZA UANACHAMA WA EAC

Rais wa Sudani Kusini, Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akipita katikati ya gwaride la Jeshi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya kutiliana saini kwa kujiunga na umoja wa Afrika Mashariki 

.
Rais wa Sudani Kusini, Jenerali, Salva Kiir Mayardit (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga (wa kwanza kulia) mara ya baada kumpokea Rais wa Sudani Kusini, Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja.


Rais wa Sudani Kusini, Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye kofia nyeusi) akishuka katika ndege ya Shirika la Kenya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages