Breaking News

Your Ad Spot

May 18, 2016

AFYA: ASILIMIA 97 YA MAJI YA UKANDA WA GAZA SI SAFI NA SALAMA

Idara ya Maji ya Palestina imetangaza kuwa zaidi ya asilimia 97 ya maji ya Ukanda wa Gaza hayafai kutumiwa kwa kunywa.

Huku ikifafanua kuwa asilimia 97 ya maji ya visima vya chini ya ardhi ya Ukanda wa Gaza yamechafuka, Idara ya Maji ya Palestina imesisitiza kuwa maji hayo si safi na salama kwa kunywa.

Vyanzo vya maji vya Ukanda wa Gaza vinakidhi mahitaji ya chini ya asilimia 25 ya wakaazi wa eneo hilo.

Kuendelea mzingiro uliowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Gaza kumezuia kujengwa mtambo wa kusafishia maji ya eneo hilo.

Idara ya Maji ya Palestina imebainisha pia kuwa utawala haramu wa Israel ndio unaodhibiti vyanzo vya maji ya Ukanda wa Gaza na kufafanua kwamba kutokana na hali ya kijiografia ya eneo hilo, utawala huo ghasibu unao uwezo wa kuchota kiwango chochote cha maji ya visima vya pamoja vya maji ya chini ya ardhi.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) maji ya Gaza yamechafuka kwa makumi ya kiwango kinachokubalika.
Aidha Umoja wa Mataifa ulitangaza katika ripoti yake ya mwaka uliopita wa 2015 kuwa endapo hali ya sasa ya Gaza haitobadilika, ifikapo mwaka 2020 eneo hilo halitoweza kukalika. Eneo la Ukanda wa Gaza lina idadi ya watu wapatao milioni moja na laki tisa.../

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages