Afisa
Usajili Kitengo cha Ubora wa Kadi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Jemima
Mulokozi (kushoto) akimuonyesha vitambulisho vilivyokamilika vikiwa na ubora
unaohitajika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali
Projest Rwegasira (katikati). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk.
Modestus Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka
hiyo, jijini Dar es Salaam Mei 28, 2016.(Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Afisa
Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Ansigar Chilemba akitoa maelezo
jinsi taarifa za muombaji wa Kitambulisho cha Taifa zinavyohakikiwa, kwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
(kulia). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA), Dk. Modestus Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi
za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam
NA
FELIX MWAGARA, MOHA
KATIBU
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
amesema fedha za kuwalipa watumishi 597 waliositishiwa mikataba yao katika
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) zipo na watalipwa hivi karibuni.
Rwegasira
alisema kiasi cha shilingi bilioni 2.3 zimetengwa kwa ajili ya malipo ya Watumishi
hao waliachishwa kazi Machi 7, 2016 ambapo wanaidai Mamlaka mishahara ya miezi
mitatu nyuma, malimbikizo ya fedha katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na makato
ya fedha za Bima ya Afya.
Akuzungumza
na watumishi wa Makao Makuu ya NIDA pamoja na Maafisa Wasajili wa Vitambulisho vya
Taifa, jijini Dar es Salaam jana, Rwegasira aliwataka watumishi hao
waliositishiwa mikataba yao, wasipotoshwe na mtu yeyote kuhusu kutokulipwa haki
zao kwani wapo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha taratibu ndogo ndogo kabla ya kuanza kuwalipa.
“Naomba
muwaambie waondoe wasiwasi wowote, waache maneno, watulie kwani Serikali ipo
makini na fedha tunazo na tutaanza kuwalipa mara tumalizapo taratibu ndogo
ndogo zilizobaki.” Alisema Rwegasira.
Aidha,
Rwegasira aliwataka watumishi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii na
kuhakikisha ifikapo Desemba 31 mwaka huu Watanzania Milioni 23 wanatakiwa
watambuliwe na kupata namba kabla ya kuanza kupewa Vitambulisho vya Taifa.
Hata
hivyo, watumishi hao walimuakikishia Katibu Mkuu huyo, kuwa kazi hiyo ya
utambuzi itakamilika kama ilivyopangwa na
itafanyika kwa umakini mkubwa kama inavyotarajiwa.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba alimshukuru Katibu
Mkuu huyo kwa kuwatembelea na kuwatia hamasa katika kukamilisha kazi pamoja na
kufikisha lengo lao la kukamilisha utambuzi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
“Tunakuahidi
Katibu Mkuu kuwa tutatimiza lengo letu na tunakuakikishia tutafanya kazi kadiri
ya uwezo wetu tukiongozwa na kauli mbiu ya ‘hapa kazi tu’, alisema Dk.
Kipilimba
Katibu
Mkuu Rwegasira alifanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza zaidi shughuli
mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka, hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na
watumishi wa Mamlaka hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
(kulia) akimsalimia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA), Dk. Modestus Kipilimba, wakati alipokuwa anawasili katika ofisi za
Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269