Real
Madrid wametwaa taji la ubingwa wa vilabu bingwa Ulaya kwa mara ya 11
baada ya kuichapa Atletico Madrid kwa mikwaju ya penati kwenye uwanja wa
San Siro mjini Milan.Bao la Sergio Ramos liliwaweka mbele vijana wa Zinedine Zidane kabla ya striker wa Atletico Antoine Griezmann hajakosa penati.Mabadiliko
yaliyofanywa na Diego Simeone kumuingiza Yannick Carrasco yaliupeleka
mchezo huo extra time baada ya kuisawazishia timu yake kipindi cha pili.Cristiano Ronaldo alipachika wavuni penati ya ushindi baada ya Juanfran kukosa penati yake kwa upande wa Atletico.Mikwaju ya penati zilivyoamua matokeaKwenye
hatua ya mikwaju ya penati, Lucas Vazquez, Marcelo na Gareth Bale
walifunga kwa upande wa Real, wakati Griezmann, Gabi na Saul
Niguezwakijibu mapigo na kufanya matokeo ya penati kuwa 3-3.Baada
ya Ramos kuifungia Real mkwaju wan ne wa penati, na kufanya matokeo
kuwa 4-3, Juanfran wa Atletico akagonshwa mwamba penati yake iliyokuwa
ya nne kwa upande wa Atletico na kutoa nafasi kwa Ronaldo kushinda taji.
Mfungaji
huyo bora wa muda wote wa mashindano akaizamisha wavuni penati yake na
kufanikiwa kushinda taji la Champions League kwa mara ya tatu kama
mchezaji binafsi kufuatia kutwaa taji hilo mwaka 2008 akiwa Manchester
United, mwaka 2014 na 2016 akiwa na klabu ya Real Madrid.
Zidane amebebwa na mbinu zake
Zinedine
Zidane alishinda Champions League akiwa kama mchezaji wa Real Mdrid
mwaka 2002, amlichukua nafasi ya Rafael Benitez kama kocha mkuu mwezi
January wakati huo Real ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 4-0 na
Barcelona mwanzoni mwa msimu huku ikiwa kwenye hatihati ya kumaliza
msimu wa pili bila taji lolote.Akiwa na umri wa miaka 43, ameumaliza msimu akiwa kocha wa saba kipa Real Madrid taji la Ulaya.
Aina yake
ya uchezaji wa timu yake kwenye mchezo wa fainali, kadri kikosi chake
kilivyokuwa kikishambulia walijitahidi kuwa imara zaidi katika eneo lao
la ulinzi na kuwabana washambuliaji wa Atletico Griezmann pamoja na
Fernando Torres hususan kipindi cha kwanza.
Gareth
Bale na Ronaldo mara kadhaa walikuwa wakiruti katika eneo la katikati na
kusaidia kuzuia mipira isiwafikie Griezmann naTorres, huku Karim
Benzema pia akishuka chini kusaidia kukaba.
Atletico
walirejea kwenye ubora wao baada ya mapumziko na kuongeza presha kubwa
golini kwa Real iliyopelekea Pepe kumchezea vibaya Torres na hatimaye
Atletico wakapata tuta huku Stefan Savic naye akipoteza nafasi ya
dhahabu.
Nini kinamsibu Diego Simeona na Atletico?
Wiki tatu
zilizopita Atletico walikuwa uwanjani wakicheza mechi ya ligi kujaribu
kupambana kuona kama wanaweza kuufukuzia ubingwa wa La Liga, lakini
kikosi cha Diego Simeone kimemaliza msimu huu kikiwa mikono mitupu baada
ya kushindwa kutwaa ubingwa dakika za mwisho.
Wakiwa
wamemaliza pointi tatu nyuma ya mabibwa wa La Liga FC Barcelona,
wameachwa na maumivu tena kwenye fainali ya Champions League licha ya
kuonesha kiwango cha hali ya juu katika kpindi cha pili ndani ya uwanja
wa San Siro.
Griezmann
aliendelea kuwa hatari kadri muda ulivyokuwa unasonga mbele, lakini
kukosa kwake penati muhimu bado ilikuwa ni pigo kwa Atletico licha ya
kwamba Carrasco baadaye aliisawazishia Atletico kwa kuunganisha krosi
tamu ya Juanfran.
Ni mara
ya tatu Atletico wamefika hatua ya fainali na kushindwa kulibakisha
kombe. Simeone anatarajiwa kuendelea kukinoa kikosi cha Atletico kwa
masimu ujao japo kuna vilabu vya England japo kuna vilabu vya Premier
League vimeonesha nia ya kutahitaji huduma yake.
Kazi yake
kubwa katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa ni kujaribu
kuwabakisha nyota wake kama Griezmann, Saul Niguez ambao tayari
wanahusishwa na vilabu vya Chelsea pamoja na Manchester United.
Clattenburg anastahili pongezi
Mwamuzi
wa England Mark Clattenburg ametekeleza majukumu yake kwa ufanisi wa
hali ya juu kwa kuumudu mchezo wa derby ulioshuhudiwa kadi nane za njano
zikitoka.
Beki wa
Real Pepe alijaribu kumshawishi mwamuzi huyo wa EPL kufanya maamuzi
ambayo yasingekuwa sahihi, lakini mwamuzi huyo pia alijaribu kumtuliza
boss wa Atletico Madrid Diego Simeone baada ya Dani Carvajal kumchezea
faulo Griezmann mapema kipindi cha kwanza.
Ramos
aliipa goli la uongozi Real ambalo kwa namna flani lilikuwa likidhaniwa
niwa ni la kuotea lakini msaidizi wa Clattenburg hakunyanyua kibendera
na hiyo ilimaanisha lilikuwa goli halali.
Hata
hivyo refa huyo ambaye pia yupo kwenye orodha ya waamuzi watakaochezesha
michuano ya Euro 2016, alikuwa sahihi kutoa penati ambayo Griezmann
alishindwa kuukwamisha mpira kambani kuisawazishia timu yake dakika ya
47.
Usipitwe na takwimu hizi muhimu
Atletico
sasa imekuwa ni klabu iliyofika mara nyingi (mara tatu) kwenye fainali
ya European Cup/Champions League na kushindwa kutwaa taji hilo
Hii ilikuwa ni fainali ya nane ya Champions League kufika hadi extra-time, nay a saba kuamuliwa kwa mikwaju ya penati.
Zinedine
Zidane ni kocha wa pili (baada ya Miguel Munoz) kushinda la European
Cup/Champions League akiwa kama mchezaji na baadaye kocha wa Real
Madrid.
Zinedine Zidane ni kocha wa kwanza kutoka Ufaransa kushinda Champions League.
Sergio
Ramos amekuwa mchezaji wa tano kufunga kwenye michezo miwili tofauti ya
fainali ya Champions League huku akiwa beki wa kwanza kufanya hivyo
(Raul, Samuel Eto’o, Lionel Messi and Cristiano Ronaldo).
Ramos
ameungana na Messi pamoja na Eto’o akiwa miongoni mwa wachezaji watatu
kufunga magoli kwenye fainali zao mbili za kwanza za Champions League.
Antoine
Griezmann amekuwa mchezaji wa kwanza kukosa penati kabla ya zile za
kutafuta mshindi kwa changamoto ya matuta. Mara ya mwisho Arjen Robben
alifanya hivyo mwaka 2012 dhidi ya Chelsea.
Marcello Lippi ndiye kocha aliyepoteza fainali nyingi za Champions League (tatu) akifatiwa na Diego Simeone (mbili).
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269