Mkuu
wa Shule ya Tiba katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili
(MUHAS), Prof. Slyvia Kaaya (wa nne kulia) akizungumza machache kabla ya
kukabidhiwa rasmi viti 200 na uongozi wa kampuni ya MeTL. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni ya MeTL, Murtaza Dewji.
Kwa
kutambua umuhimu wa elimu, kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania
Limited (MeTL Group) imetoa msaada wa Milioni 30.7 kwa Chuo Kikuu cha
Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) ili kusaidia ununuzi wa viti 200
ambavyo vitatumiwa na wanafunzi wa udaktari wa watoto.
Akizungumza na Modewjiblog
kuhusu msaada huo, Mkuu wa Shule ya Tiba katika Chuo Kikuu cha Sayansi
na Tiba Muhimbili (MUHAS), Prof. Slyvia Kaaya, amesema kabla ya kupata
msaada huo walikuwa wakitumia chumba kidogo ambacho kilikuwa hakiwatoshi
wanafunzi wanaosomea udaktari wa watoto hivyo msaada huo umekuwa muhimu
kwao ili kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.
“Msaada
huu utatusaidia sana na hata sasa hivi tuna matarajio tutakuwa na
matokeo mazuri kwa kuongezeka kwa watahiniwa, wanafunzi kuhudhuria
vipindi na hata kwa walimu uadilifu wa kufundisha utaongezeka,” alisema
Prof. Kaaya.
Aidha
Prof. Kaaya alisema pamoja na msaada huo lakini bado wanachangamoto
ambazo zinawakabili ambazo zinahitaji kutafutiwa ufumbuzi ikiwa ni
pamoja na kufunga viyoyozi na kuweka mitambo ya kuzuia mwangwi ili
kuwawezesha wanafunzi kusoma bila kuwa na matatizo.
Nae
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer alisema kampuni
yao imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwa jamii ili kusaidiana na
serikali kumaliza baadhi ya changamoto zilizopo na wamejipanga kuendelea
kuwa wakitoa misaada kwa wahitaji.
“Tunaamini
elimu ni muhimu kwa maendeleo ya baadae tunatoa msaada ili wasome na
wawasaidie wengine kupitia elimu wanayoipata chuoni,” alisema Fatema
Dewji-Jaffer.
Mkurugenzi
wa Uendeshaji wa Kampuni ya MeTL, Murtaza Dewji (kushoto) akitoa salamu
za kampuni ya MeTL kabla ya kukabidhi viti 200 kwa uongozi wa MUHAS.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji-Jaffer.
Mkurugenzi
wa Masoko wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL),
Fatema Dewji -Jaffer (wa tatu kulia) akimkabidhi moja kati ya viti 200
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Prof.
Aporinal Kamuhangwa (wa pili kushoto) vilivyotolewa na kampuni ya MeTL
Group. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Tiba katika Chuo Kikuu cha Sayansi na
Tiba Muhimbili (MUHAS), Prof. Slyvia Kaaya. Wengine wanaoshuhudia tukio
hilo kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni ya MeTL Group,
Murtaza Dewji na Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Barbara
Gonzalez (kulia). Mstari wa nyumba ni watumishi wa Chuo Kikuu cha
Sayansi na Tiba (MUHAS).
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano yaliyofanyika katika jengo la Watoto lililopo Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kaimu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Prof.
Aporinal Kamuhangwa akitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa
kampuni ya MeTL Group, Murtaza Dewji baada ya kukabidhiwa viti hivyo.
Meneja
Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez (kulia)
akizungumza neno baada ya hafla fupi ya kukabidhi viti hivyo.
Uongozi wa MeTL na MUHAS wakiwa wamekaa kwenye viti hivyo.
Mkurugenzi
wa Masoko wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL),
Fatema Dewji -Jaffer (katikati) akifurahi jambo na Mkurugenzi wa
Uendeshaji wa kampuni ya MeTL Group, Murtaza Dewji. Kushoto ni Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Karim Manji.
Viti 200 vya MUHAS vilivyotolewa na Kampuni MeTL.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269