Madee
BONIPHACE NGUMIJE
MKALI wa
Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’ ameweka wazi mipango ya msanii wake,
Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kuwa tayari ameshaanza kung’aa kimataifa.
Dogo Janja
Akilonga
na mtandao wa Global Publishers, Madee alisema kuwa kwa sasa Dogo Janja
anatamba na remix ya Wimbo wa My Life aliowashirikisha wakali kutoka
Uganda, Radio na Weasel na kufanya hivyo njia zinaonekana kuwa wazi.
“Natarajia
kumuona Janja kwenye levo nyingine baada ya kuibuka na remix ya My
Life. Kwa sasa atatoka na Ngoma ya Kidede iliyofanyika MJ Records na
video kushutiwa na Hanscana. Naimani njia yake itaendelea kuwa nyeupe
kimataifa,” alisema Madee.GPL(P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269