Umoja wa Afrika (AU) umeeleza kuwa utashirikiana na Somalia kudhamini usalama wakati wa kufanyika uchaguzi nchini humo.
Bi Lydia Wanyoto Naibu Mjumbe Maalumu wa Mwenyekiti wa
Kamisheni ya Umoja wa Afrika katika Masuala ya Somalia amesema kuwa
vikosi vya umoja huo (AMISOM) vitashirikiana na askari usalama wa
Somalia kukabiliana na harakati za wanamgambo wa al Shabab wenye lengo
la kuvuruga uchaguzi mkuu ujao nchini humo.
Afisa huyo wa ngazi ya juu wa Umoja wa Afrika ameongeza kuwa tayari
kumeanzishwa kikosi cha askari jeshi huko Somalia ambao watakuwa na
jukumu la kudhamini usalama wakati kutakapofanyika uchaguzi yaani mwezi
Septemba na Oktoba ujao nchini humo. Tume ya Uchaguzi ya Somalia
imetangaza kuwa uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo utafanyika tarehe 30
Oktoba na wa bunge umepangwa kufanyika kati ya tarehe 24 Septemba hadi
tarehe 10 Oktoba. Wanamgambo wa al Shabab wamekuwa wakivuruga hali ya
usalama huko Somalia kwa kutekeleza mashambulizi katika maeneo
mbalimbali nchini humo na hata dhidi ya kikosi cha kulinda amani nchini
humo (AMISOM).
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269